Habari za Punde

Maambukizo Mapya ya Ukimwi Yapungua Pemba

Na Shaibu Kifaya, Pemba.
MAAMBUKIZI mapya ya virusi vya ukimwi yamepungua kwa kiasi kikubwa kisiwani humu, kutokana na kuanzishwa kwa miradi ya nyumba maalumu za kurekebishia tabia (Sober House).

Akizungumza na makundi maalumu kilichowashirikisha viongozi wa Wilaya, katika ukumbi wa maabara ya wananchi Wawi Chakechake Pemba, Dk Maryam kutoka kitengo cha kinga Zanzibar, alisema maambukizo hayo yamepungua kutokana na watumiaji wa dawa za kulevya wanaotumia njia ya kujidunga shindano.

Aidha alisema suala la utumiaji wa madawa ya kulevya ni kichocheo kikubwa cha maambukizi ya virusi vya ukimwi na ukimwi wenyewe na kutokumpelekea mtumiaji huyo kufanya mambo yasiyofaa katika jamii bila ya kujitambua .

Hata hivyo, alisema kumekuwa na changamoto kubwa ya kuongezeka kwa watumiaji wa dawa hizo kutokana na polisi kutowakamata watu wanaotumia madawa hayo.

Nae, Dk Shaabani Hassan Haji, kutoka kitengo cha kinga Zanzibar alisema hali ya ongezeko la VVU vile vile kwa wanawake waja wazito alisema asilimia 0.6 lakini bado kumeonekana kuwa na ongezeko la maambukizi mengi kwa baadhi yao .

Nao washiriki wa mkutano huo walisema kwamba uanzishwaji wa polisi jamii katika shehia mbali mbali wamesaidia kupambana na vitendo hivyo viovu ambavyo ni hatari kwa jamii jambo ambalo lina weza kuwa shawishi kwa wana jamii wengine .

Mapema akifunga kikao hicho msaidizi meneja wa kitengo cha kinga Pemba, Abdalla Omari, alisema kunaweza kuibuka hisia tofauti kwa wananchi amao wataweza kusaidia kupambana na maambukizi ya virusi vya ukimwi ili janga hilo lisiendelee .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.