Habari za Punde

JODA Yawapiga Msasa Wanakijiji wa Jongowe



Na Mbarouk Abdulla, MCC
JUMUIYA ya Maendeleo ya kijiji cha Tumbatu Jongowe (JODA), imewataka wanachama na wananchi wa Jimbo la Tumbatu, Mkoa wa Kaskazini Unguja, kuitumia vyema elimu ya Sera na uhifadhi wa maendeleo ya mama na mtoto, ili kuleta mabadiliko katika jamii.

Afisa Maendeleo ya Vijana, Hassan Ali Kombo, alieleza hayo wakati akiwalisha mafunzo kuhusiana na mama na mtoto katika ukumbi wa Meca, Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Hassan, alisema jamii imekuwa na mapungufu ya uelewa wa sera za kitaifa, sera ya uhifadhi wa mama na mtoto na sera ya udhalilishaji wa kijinsia ya wanawake na watoto ndio maana JODA ikaamua kutoa mafunzo hayo, kwa lengo la kuilemisha jamii kutambua sera hizo.

“Tumepanga kutoa elimu hii kwa kuisaidia jamii ili iweze kutambua mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuondokana na vikwazo tofauti vinavyosababishwa na ukosefu wa elimu ya sera na haki za mama na mtoto kwa makusudi kwa lengo la kuleta mabadiliko katika jamii husika”, alisema Hassan.

Alifahamisha kuwa wakati umefika sasa jamii kuelewa haki zao na kazisimamia vizuri haki zao sambamba na kuzilinda pamoja na kujiepusha na mambo maovu ili kupnguza mtiririko wa matatizo ndani ya jamii.

Nae Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo ya kijiji cha Jongowe, Khamis Ali Khamis, alieleza kuwa, tangu walipoanza kutoa taaluma hiyo wameweza kuona mabadiliko, hata hivyo kumekuwa na changamoto katika suala la uwajibikaji katika hasa za sheria.

“Changamoto kubwa inayotukabili ni kulegalega katika utekelezaji sheria upande wa vyombo vya sheria hazijatekelezwa ipasavyo na hili linatuvunja moyo”, alisema.

Kwa upande wake mshika fedha wa Jumuiya hiyo, Bushara Mohammed Juma, alifahamisha kwa kiasi kikubwa mafunzo hayo yameleta mafanilio kwa kuwa yamepunguza vitendo vya unyanyasaji kwa akinamama na wamekuwa mstari wa mbele kushiriki shuhuli za klimaendeleo.

“Jamii itusaidie kwa kufichua mambo maovu bila ya kujali nani kafanya kosa na napenda kuchukua fursa hii kuwataka washiriki kuitumia vizuri taaluma hii”, alisema.

Mafunzo hayo yameandaliwa na (JODA) na kudhaminiwa na Foundation for Civil Society utaendelea hadi Oktoba 2012, ambapo hadi sasa umeleta mafanikio katika jamii katika vijiji vya Tumbatu, Pale, Mkokotoni, Mto wa pwani, Mto wa Maji na Kiongele vilivyo Kaskazini Unguja








No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.