Habari za Punde

Majimaji yairovya Idumu

Na Asya Hassan
MICHUANO ya Ligi ya Mabingwa Wilaya Taifa iliendelea kurindima katika viwanja viwili tafauti juzi.

Katika mchezo uliofanyika uwanja wa Polisi Ziwani, timu ya Majimaji ya Nyerere ilipambana na Idumu kutoka Unguja Ukuu, ambapo Majimaji iliibuka na ushindi wa mabao 3-1.
Majimaji ilitawala mchezo huo kwa muda wote na kuwaweka katika wakati mgumu wapinzani wao.

Licha ya jitihada za Idumu kutaka kusawazisha mabao hayo, mambo yalionekana kuwaendea kombo na kulazimika kusalimu amri.

Aidha uwanja wa Mao Dzedong, timu ya DESI kutoka Dole Wilaya ya Magharibi, ilitoshana nguvu kwa sare isiyo na magoli dhidi ya Victoria kutoka Donge Mnyimbi.

Katika mchezo huo timu zote zilioneshana ufundi huku kila moja ikitaka kujipatia bao, lakini timu hizo zilijikuta zikimaliza dakika 90, bila kupatikana mbabe.

Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea tena kesho kwenye uwanja wa Mao Dzedong kwa mchezo utakaozikutanisha timu za DESI na Majimaji.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.