Na Mwandishi wetu, DAR ES SALAAM
BARAZA la Taifa la Mitihani Tanzania (NECTA), jana liliweka hadharani matokeo ya kidato cha sita ya mwaka 2012, ambaya yaonesha kuwa skuli za Zanzibar kama kawaida zimeendelea kushindwa kuwika.
Kwa mujibu wa muhtasari wa matokeo hayo yaliyotolewa na jana na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dk. Joyce Ndalichako, yameonesha kuwa katika kundi la skuli 10 zilizofanya vibaya sana zenye watahiniwa 30 na zaidi skuli za Zanzibar ni saba.
Skuli hizo ni pamoja na Pemba Islamic Collage, Zanzibar Commercial, Uweleni, Mazizini, Lumumba, Laurent International na Haile Selassie.
Aidha katika kundi la skuli za mwisho zenye watahiniwa chini ya 30 Zanzibar imeingiza skuli tano ambazo ni Mbarali Preparatory, Philter Federal International, High View International, Sha na Al - Falaah Muslim.
Wanafunzi bora watano bora kitaifa wa masomo ya sayansi ni Faith P. Assenga kutoka skuli ya Marian Girls ya Pwani, Zawadi N. Mdoe kutoka Feza Boy’s, Dar es Saalam, Belnadino Mgimba kutoka skuli ya Minaki Pwani, Jamal Juma Feza Boy’s Dar es Salaam na Imaculate R. Mosha kutoka Marian Girls Pwani.
Watahiniwa watano bora kitaifa masomo ya biashara Alex M Isdor kutoka Kibaha Pwani, Ephraim Tumwiduke St.Joseph Cathedral Dar es Salaam, Vaileth Mussa Weruweru Kilimanjaro, Suleimani Manyiwa Kihaba Pwani na Hussein Issa Azania Dar es Salaam.
Wanafunzi watano bora kitaifa masomo ya lugha na sayansi ya jamii Faridi Abdalla kutoka Mpwapwa Dodoma, Hemedy Hussein Tasomaganga Iringa, Anselimo C. Mlimbo Madibira Mbeya, Elibaraka A. Mmari Lyamungo Kilimanjaro na Salvatory R. Kessy Majengo Kilimanjaro.
Katika matokeo hayo watahiniwa 51 yamezuiliwa kutokana na kutolipa ada ya mitihani ambapo mara tu watakapolipa fedha hizo hawatasita kupwatiwa matokeo hayo.
Aidha watahiniwa watatu wa skuli na watahiniwa watatu wa kujitegemea wamefutiwa matokeo kutokana na udanganyifu.
Katika hatua nyengine NECTA), limewapa shufaa watahiniwa wa kidato cha nne waliobainika kuchakachua mitihani ya kidato cha nne ya mwaka 2011 ambapo jumla ya wanafunzi 3,303 walizuiwa kutofanya mitihani hiyo kwa muda wa miaka mitatu.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) Dk. Joyce Ndalichako, alisema kutokana na kilio cha wadau mbali mbali adhabu hiyo imepunguzwa kutoka miaka mitatu hadi mwaka mmoja.
Alisema katika mkutano wa 87 uliokutana Aprili 30 mwaka huu, uliamua kupunguza adhabu hiyo kutoka miaka mitatu hadi mwaka mmoja, ambapo wanafunzi hao wataruhusiwa kufanya mitihani kama wanafunzi wa kujitegemea mwaka 2013.
Alisema kikao hicho kimepounguza adhabu hiyo baada ya wahiniwa na wadau wengine walioathithirika na adhabu hiyo kuomba msamaha na kwamba wametambua athari zinazoweza kuwakumba pale wanabainika kuchakachua mitihani.
Katika taarifa hiyo Ndalichako alisema kuwa Baraza hilo haliwezi kuvumilia udanganyifu katika mitihani na kwamba na kwamba atakayebainika adhabu ya kufutiwa matokeo itatekelezwa kuzuiliwa kufanya mitihani itaendelea.
Wakati huo huo, katibu huyo wa NECTA, alisema kuwa baraza lake limeshauri hatua zichukuliwe kwa maofisa wote walioshiriki na kuchangia udanganyifu wa mitihani ya kidato cha nne.
Dk. Ndalichako alieleza hayo jana jijini Dar es Salaam alipokuwa akitoa muhutasari wa mtokeo ya kidato cha sita kwa waandishi wa habari na kuelezea matokeo ya kamati iliyoundwa kuchunguza kadhia ya udanyanyifu kwenye mitihani ya kidato cha nne.
Katibu huyo alisema baraza hilo litapitia kanuni zake kwa lengo la kuhakikisha linaziba mianya ya udanganyifu hasa baada ya kujitokeza watahiniwa kuchelewa kwa nusu saa kuingia katika vyumba vya mitihani.
Akizungumzia yaliyojitokezea kufuatia uchunguzi wa kamati hiyo, Dk. Ndalichako alisema ilibainika kuwepo kwa wasimamizi wa mitihani wenye sifa ambao walichangia kujitokeza kwa udanganyifu kwenye mihani hiyo.
Aidha tatizo jengine lililobainika ni la walimu kupangiwa kusimamia mitihani katika skuli wanazofunmdisha, huku pia katika baadhi ya wilaya walikuwepo askari polisi na wasimamizi waliochukua mitihani kwenye ‘strong room’ ya mkoa asubuhi na kupeleka katika vituo jukumu ambalo lilipaswa kufanywa na kamati za wilaya.
Katika uchunguzi huo uliofanywa kwa skuli za Bara na Zanzibar, pia ulibaini wasimamizi wa mitihani hawakuaa ndani ya vyumba vya mitihani kwa muda wote hali iliyowapa mwanya watahiniwa kufanya udanganyifu.
Hili ndio la tatizo la kufungua Form 5 na 5 kila kona bila ya kuwa na walimu wenye sifa. Hakuna miujiza wanautumia wanaopasi. Ukiwa na walimu wenye sifa na walio makini basi lazima wanafunzi watapasi. Hii trend ya kufeli itaendelea kila siku.
ReplyDeletePoleni.