Habari za Punde

Reli ya Zanzibar wakati huooo.......................

Mdau mambo ya Reli wakati huo unaweza ukasema iko mahali gani ikipita hii reli mdau wngu.

6 comments:

  1. hapo ni kwenye daraja baina ya M/kumbi na Saateni au nimekosea?jengo unaloliona kama sikosei ni kambi ya jeshi

    ReplyDelete
  2. Duu...!,kaka hizi picha mnazitoa wapi?..Nadhani hili ni lile daraja la kupandishia Mtoni kwa kisasi.

    ReplyDelete
  3. Mtoa maoni wa kwana naona umepatia , hilo jumba nafikiria ni jumba la mle JKU

    ReplyDelete
  4. sasa Jamani munasifu mambo ya kale, hivi sasa yako wapi ? Au ndio faida za muungano kila kitu kimemezwa. Ah sisi innallillah.................

    ReplyDelete
  5. Hapa zaidi tunaangalia gharama za ujinga (kukosa elimu) kwa watawala wa wakati huo( waarabu) na namna ilivyoigharimu Z'bar!

    Hivi inakuwaje kuwa na nchi tajiri kiasi hicho kwa wakati huo halafu tukaishia kuwa maskini wa kutupwa?

    Nasema ni ujinga kwasababu inasemekana uchumi wa visiwani ulianza kuporomoka kidogo kidogo kutokana na ujinga wa 'wamanga' na kupenda starehe na baada ya mapinduzi wazee wetu tena wakaja kumalizia!

    Inasemekana hata hiyo reli ilikufa 1927, na watu walishindwa hata kutunza yale mataruma ili yawe kumbukumbu kwa kizsazi kijacho na kituo chake cha mwisho kilikuwa mle ngome kongwe..elimu bwana?

    Ndio maana tukaambiwa..

    -IKRAA!!

    -INNA MA YAKHSHA LLAH MIN IBADIHI AL ULAMAA!

    -HAL YASTAWI ALLADHINA YAGHLAMUNA WA LLADHINA.. LA.. YAGHLAMUUN?

    ReplyDelete
  6. Kaka picha za Z'bar ya kale ukipata nyingine naomba utuwekee, zinakumbusha machungu lakini pia zinafuraisha.
    Lile jumba mle jku naskia ilikua Agakhani club, na lilikua moja ya majumba matata ya wakati huo lakini wapi? kama ilivyo kwa palace ya chukwani. wahadimu wamewaachia majeshi wayavunje!

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.