Habari za Punde

Watoto watakiwa kulelewa kwa maadili ya kidini

Na Halima Omar, MMG
WAZAZI na Walezi nchini wametakiwa kutoa malezi bora kwa watoto wao ili kupatikana kwa kizazi bora cha baadae.

Akizungumza katika shura ya kuwahamasisha wanawake wa kiislamu katika ukumbi wa Al-madrasati Nasir Muslimina Kianga wilaya ya magharibi Unguja, Sheikh Abdalla Mnubi Abasi Amiri, kutoka Jumuia ya Vijana wa kiislamu Zanzibar, alisema ili kuona kwamba walezi wanalelewa malezi bora ya kiislamu jamii haina budi kufuata misingi ya dini hiyo.

Alisema wakati umefika sasa kwa walezi kuwa imara na kwamba wasiwaridhie watoto kwa mambo yanayokwenda kinyume na maadili ya dini ya kiislamu.

“Malezi wanayopatiwa watoto hayajawa ni kigezo cha kuwafanya wazazi warizike nayo ni lazimza kusimama imara ili kuhakikisha wanatoa malezi bora yenye kufuwata mwenendo mzima wa dini yao na misisngi ya tawhidi”, alisema Sheikh huyo.

Sheikh Mnubi alisema kuwa mtoto ni hazina hivyo wazazi na walezi wafahamu maisha mazuri kwa mtoto yanahitaji malezi bora ambayo yatamjengea heshima katika jamii na taifa kwa ujumla.

Hata hivyo, Sheikh Mnubi, aliwaasa wazazi na walezi hao kuwapa fursa ya kuwasikiliza watoto wao wanayosema kwani wanahaki na wajibu wa kusikilizwa na kutoa mchango wao katika jamii kama walivyo watu wengine.

Aidha aliwataka wazazi na walezi kuwahamasisha vijana kuachana na tabia ya kujiingiza katika vikundi viovu kwani vinaathiri afya na kurudisha nyuma maendeleo vijana ukizangatia vijana ndio taifa la kesho.

Nae Amiri msaidizi kutoka kanda ya Kianga, Naima Nasour, akichangia shura hiyo alisema kukosekana kwa malezi bora yanachangiwa na baadhi ya wazazi wa kiume kushindwa kutoa mchango wao na kuachiwa majukumu wazazi wa kike peke yao hali ambayo hukosekana kizazi bora.

Hata hivyo Amiri Naima alitoa wito kwa wazazi wakiume kushirikiana kwa pamoja ili kurudisha malezi ya asili na kutunza silka na utamaduni wa mzanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.