Habari za Punde

Zanzibar Triathlon Kutimua Vumbi Zenj.

Na Mwajuma Juma
MASHINDANO ya Trithlon kitaifa, yanayotarajiwa kufanyika leo yakihusisha mchuabno wa kuogelea, resi a baiskeli na mbio za nusu marathoni, ambapo yatarindima kwenye viunga vya hoteli ya Mtoni Marine asubuhi hii.

Katibu Msaidizi wa Chama cha Mchezo huo Zanzibar Ali Abdallah Aminie, ameliambia Zanzibar Leo kuwa, maandal;izi yote ya mashindano hayo yamekamilika na yatashirikisha timu za Unguja pekee, sambamba na wachezaji wawili kutoka Italia.

Michuano hiyo imeandaliwa kwa lengo la kuifufua baada ya kupotea kwa zaidi ya miaka tisa sasa ambapo zamani ilikuwa ikiandaliwa na Kamisheni ya Utalii Zanzibar kwa kushirikiana na Chama cha Riadha Zanzibar (ZAAA)..

Alifahamisha kuwa, washindi wa mashindano hayo watapewa zawadi
kwa kuanzia mshindi wa kwanza hadi watano, sambamba na washiriki wote kupewa
kifuta jasho cha shilingi 20,000 kila mmoja.

Alisema mchuano wa kuogolea utakuwa wa kilomita moja na nusu, baskeli kilomita 40 kutoka Mtoni Marine mpaka Bumbwini na kurudi, huku mbio za nusu marathoni, washiriki watafukuzana kwa masafa ya kilomita kumi kutoka Mtoni

Marine kupitia Saateni, Mikunguni, Amani, barabara ya Mkapa na kumalizia Mtoni Marine.

Washindi wa kwanza katika kila mchezo, watazawadiwa shilingi 70,000, wa pili 60,000, na watakaoshika nafasi za tatu wataondoka na shilingi 50,000, wa nne 40,000 na watano
watapata shilingi 35,000 kila mmoja.

Klabu zinazotarajiwa kushiriki patashika hiyo, ni Jeshi, KMKM, Polisi, Wilaya ya
Kaskazini A, Wilaya ya Magharibi, Kombeni na Forodhani.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.