Harakati za biashara katika mitaa ya Darajani ikishamiri. mdau
Mgahawa uliokuwa katika bustani ya Foro ukiwa umeaguka sehemu moja ya paa lake kwa kukaa kwa muda mrefu bila ya kutoa huduma hiyo na kupata kadhia hiyo na kuondosha haiba ya uzuri wa bustani hiyo inayotembelewa na watu wengi wakati wa jioni kwa ajili ya kujipumzisha na kupunga hewa ya bahari.
Hivi ndivyo unavyoonekana baada ya kuanguka sehemu ya moja ya paa lake.
Ukionekana sehemu ya baharini ambapo sehemu kubwa iko katika bahari, ulikuwa kivutio kwa wageni wanaofika katika bustani hiyo. umesimama siku nyingi kutoa huduma wakati wa ujenzi wa bustani hiyo, ndipo upoaza kusimama kutowa huduma za chakula na vinywaji.Unahitaji upate ufumbuzi wa haraka kunusuru hali hiyo usiendelee kuharibika kwa kuanguka katika kipindi hicha cha jua kitasababisha kuendelea kuoza mbao zake baada ya kupigwa na mvua za masika zilizomalizika hivi karibuni.
Haya ni matokeo ya viongozi wasiwo na ujasiri!
ReplyDeleteHuwezi kuacha 'karakacha ' kama hilo mbele ya uso wa nchi.
Eti kisingizio kuna kesi mahakamani! serikali ina namna nyingi ya kutatua mgogoro wa namna hii.
Kazi..kweli ..kweli!