Na Mwashamba Juma
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Fatma Abdul- Habib Ferej, amesema umefika wakati kila Mzanzibari kujitathmini na kutafakari kwa kiasi gani harakati zake zinatunza na kuhifadhi mazingira.
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Fatma Abdul- Habib Ferej, amesema umefika wakati kila Mzanzibari kujitathmini na kutafakari kwa kiasi gani harakati zake zinatunza na kuhifadhi mazingira.
Waziri huyo alieleza hayo jana ofisini kwake Migombani mjini Zanzibar, alipokuwa akitoa taarifa maalum ya serikali ya siku ya Mazingira dunia ambayo huadhimisha kila ifikapo Juni 5 ya kila mwaka.
Alisema kutokana na athari za kimazingira kila mwananchi anapaswa kutafakari ni kwa kiasi gani shughuli zake za kujitafutia riziki zinatoa umuhimu wa kuhifadhi mazingira.
"Katika visiwa vyetu vya Zanzibar kuna idadi ndogo ya watu ambao wanajali utunzaji na uhifadhi wa mazingira katika shughuli zao za kila siku za kujitafutia maisha",alisema waziri huyo.
Alisema kuendelea kupuuza uhifadhi na utunzaji wa mazingira ni hatari kwa Zanzibar hasa ikizingatiwa kuwa ni visiwa ambavyo vina maliasili chache zinazohitajika katika maendeleo ya maisha kwa vizazi vilivyopo na vijavyo.
Waziri huyo alisema uchafuzi wa mazingira unatokana na kuweka makaazi kwenye vianzio vya maji, na kujenga katika ardhi za kilimo, jambo ambalo huua uchumi endelevu na kuiharibu ardhi ambayo itazalisha kwa wingi.
Aliongeza kuwa ukataji miti ovyo, uchimbaji wa mchanga, kokoto, mawe na udongo kiholela pamoja na ujenzi usiokuwa na mpangilio ni miongaoni mwa changamoto zinazosababisha uharibifu wa mazingira ambapo athari zake ni kubwa.
Alifahamisha kuwa utupaji taka kiholela za majumbani, mahotelini na sehemu za biashara, kuendelea kutumia mifuko ya plastiki pamoja na uingizaji wa bidhaa chakavu ‘e-west’ pia ni visababishi vya uchafuzi wa mazingira.
Akizungumzia athari zinazotokana na mabadiko ya tabia nchi, waziri huyo alisema ukame wa muda mrefu na mong’onyoko wa fukwe za bahari ni miongoni mwa athari za mabadiliko ya tabia nchi zinazosababishwa na kuchangia kwa kiasi kikubwa cha uharibifu wa mazingira.
Aidha waziri huyo aliwataka wananchi kurejesha utamaduni wa zamani wa kuhifadhi taka katika sehemu maalum mara baada ya kusafisha maeneo yao, ili kujilinda na maradhi mbalimbali yanayoweza kuonoda uhai wetu.
Sambamba na kuwataka wavuvi kuachana na uvuvi haramu katika maeneo mbalimbali ya visiwa vya Unguja na Pemba ili huyanusuru matumbawe na samaki wanyanga visiathiriwe na uharibifu huo.
Siku ya mazingira huadhimishwa duniani kote kila ifikapo Juni 5 ya kila mwaka, ambapo maadhimisho ya siku hiyo yalianzishwa na Umoja wa Mataifa mwaka 1972 huko Stockholm nchini Sweden.
Kwa Zanzibar maadhimisho ya siku hii yanafanyika leo katika viwanya vya Gombani Chakechake Pemba ambapo jumbe wa mwaka huu ni "Uchumi Endelevu, Je, unakuhusu wewe?"
No comments:
Post a Comment