Habari za Punde

Tume ya Kukusanya Maoni ya Katiba ikiwa katika Kijiji cha Michamvi na Kibuteni Wilaya ya Kusini Unguja.

Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ya Tanzania Balozi Dk. Salim Ahmed Salim, akizungumza machache kuhusiana na Mabadiliko ya Katiba katika Kijiji cha Michamvi Wilaya ya Kusini Unguja, walipofika kukusany maoni ya Wananchi kuhusu Katiba.
Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Richard Limo, akielezea  mutasari wa kutowa maoni kwa Wananchi wa Michamvi, Wilaya ya Kusini Unguja Mkoa wa Kusini.

Wananchi wa Kijiji cha Michamvi Wilaya ya Kusini Unguja, wakiwa katika Viwanja vya Skuli ya Michamvi wakisikiliza maoni ya baadhi ya Wananchi wakiwasilisha katika Tume iliofika kuchukuwa maoni ya Wananchi wa Mko wa Kusini Unguja. 
Mwananchi wa Kijiji cha Michamvi akichangia maoni yake mbele ya Tume, kitaka Serekali mbili na kuondoa kero za Muungano na kutaka Muungano Udumu
Wananchi wa Kijiji cha Michamvi wakiende kutowa maoni yao mbele ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilipofika katika Kijiji hicho skuli ya Michamvi.

Mwanamchi wa Kijiji cha Michamviakichangia maoni yake mbele ya Tume ya Mabadiliko ya Katika Mpya ya Tanzania.

Mwananchi wa Kijiji cha Michamvi, akitowa maoni yake kuhusu mabadiliko ya Katiba. Na kusema Serekali ya Muungano iendelee kudumishwa na Umedumu kwa miaka 48 sasa.Amesema Rais wa Zanzibar lazima awe na pande nane za kuzaliwa ikimaanisha awe mzaliw w Zanzibar kwa pande zote, pia ametaka kuondolewa kwa kero za Muungano za muda mrefu na ametaka muundo wa serekali ziwe mbili.       

Wananchi wa Kijiji cha Michamvi wakisikiliza maoni ya Wananchi wanayoyatoa kwa Tume katika viwanja vya skuli ya Michamvi. 

Mwananchi wa Kijiji cha Kibuteni Makunduchi akichangia maoni yake mbele ya Tume ya Mabadiliko ya Katibu.
Mwananchi y Kijiji cha Kibuteni Makunduchi akitowa maoni na mengi yakiwa katika barua aliyakabidhi katika meza ya Tume, walipofika katika viwanja vya skuli ya Kibuteni

Wananchi wa Kijiji cha Kibuteni Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja wakiwa katika viwanja vya skuli ya kibuteni wakisikiliza maoni yanayotolewa na Wananchi.



No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.