Habari za Punde

Dk Shein Amwapisha Waziri mpya wa Miundombinu na Mawasiliano leo


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimuapisha Rashid Seif Suleiman kuwa Waziri waMiundombinu na Mawasiliano,katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar Leo

Na Rajab Mkasaba, Ikulu

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein leo amemuwaapisha Mhe.Rashid Seif Suleiman kuwa Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Hamad Masoud Hamad.

Wakati huo huo, Dk. Shein amemuapisha Sheikh Daud Khamis Salim kuwa Kadhi wa Rufaa  Pemba. Sheikh Daud aliteuliwa Mei 26 mwaka huu.


Hafla hiyo ilifanyika Ikulu mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali akiwemo Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Balozi Seif Ali Idd, Spika wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Pandu Ameir Kificho, Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe.Omar Othman Makungu,  Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud.

Wengine ni Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabih, Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Abdalla Mwinyi Khamis, Meya wa Manispaa ya Mji wa Zanzibar, Mstahiki Khatib Abdulrahman Khatib, Washauri wa Rais, Naibu Waziri wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Mhe. Issa Haji, Naibu Mufti Sheikh Mahmoud Wadi, Naibu Kadhi Sheikh Hassan Othman Ngwali pamoja na viongozi wengine.

Dk. Shein jana tarehe 23 Julai 2012, alikubali ombi la Mhe. Hamad Masoud Hamad la kutaka kujiuzulu ili awajibike kisiasa kutokana na ajali ya kuzama kwa meli ya MV Skagit iliotokea tarehe 18 Julai, 2012  ambayo ilisababisha vifo na majeruhi kadhaa.

Kutokana nakujiuzulu huko kwa Mhe. Hamad, Dk. Shein alimteua Mhe. Rashid Seif Suleiman kuwa Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

2 comments:

  1. Maendeleo yatapatikana vipi,viongozi wote wamekwenda kuhudhuria kuapishwa Waziri mpya sasa nani atafanya kazi zao au hii ndio kazi.

    ReplyDelete
  2. Dali zote zinaashiri kua wawakilishi wengi wa CUF ni wale wanaolipwa fadhila za kuhangaikia chama mda merfu, vinginevyo huyu mzee angeachwa apumueee!

    Ukimuangalia tu unapata picha, wizara itakua na hali gani!...naona kama ni yale yalee!!!

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.