Habari za Punde

Dk Shein Anena - Meli Inunuliwe

Aiagiza Wizara ya Fedha kusaka fedha 

Na Rajab Mkasaba, Ikulu

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, ameiagiza Wizara ya Nchi Afisi ya Rais Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo kuandaa utaratibu wa kupata fedha ndani ya wiki moja kwa ajili ya kununua meli kubwa mpya ya abiria wapatao 1000 na yenye uwezo wa kuchukua mizigo ya tani 100. 

 Dk. Shein ametoa agizo hilo leo wakati alipokuwa na mazungumzo na uongozi wa Shirika la Meli pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Shirika hilo ambapo pia kikao hicho kilihudhuriwa na uongozi wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano na Wizara ya Nchi Afisi ya Rais Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo. Katika kikao hicho maalum 


Dk. Shein ameiagiza Wizara hiyo kutafuta fedha hizo kutokana na vianzio vya ndani au nje ya nchi ama kutokana na taasisi zinazohusiana na mambo ya fedha. 

 Alieleza kuwa katika kipindi kisichozidi miezi miwili ujumbe maalum uende kwa Kampuni zinazotengeneza meli nchini Korea Kusini, China au Japan kwa ajili ya kuwasilisha fedha za utangulizi kwa ajili ya ujenzi wa meli hiyo. 

 Mapema uongozi wa Shirika la Meli, ulimueleza Dk. Shein kuwa kwa kawaida ujenzi wa meli yenye ukubwa huo, huchukua mwaka mmoja kukamilika. 

 Kikao hicho ambacho kilikuwa na lengo la kuangalia mwelekeo na Mipango ya Shirika la Meli pia, kilijadili hali halisi ya meli za Shirika la Meli na baadae kujadili masuala ya ununuzi wa meli mpya itokayowaondoshea usumbufu wa usafiri wa baharini wananchi wanaosafiri kati ya Unguja, Pemba na Tanzania Bara.

2 comments:

  1. Kwa mara ya kwanza nimeona amri ya Rais iliyojaa hisia na machungu ya kujali wananchi wake.

    Nilishaingiwa kigugumizi baada ya kusikia meli au boti tatu zimeshafutiwa usajili bila ya kuwa na badili. Maana yake ni usumbufu wa ziada kwa wasafiri hasa wenye kipato cha chini.

    Thank you Mr President

    ReplyDelete
    Replies
    1. Dear Mr Anonymous,
      Your thank you to Mr President is no thank you!
      Hii ndio shida yetu Wazanzibari, kwani hatuoni jizani mpaka moto uwake. We always tend to put off fires and not work towards preventing fires.
      Hivyo serikali ilikuwa haijui kama maafa kama haya tutakuwa tunapata? Before 1964 hatujawahi kupata maafa kama haya, kwasababu serikali was incharge, lakini sikuhizi nobody is incharge. Tunawaachia wanyonyaji na boti zao ndogo kutupotezea maisha yetu tu. Serikali ilikuwa tokea kuondoka MV Mapinduzi itafute chombo chengine cha maana na sio tungojee mpaka maafa yashatufika ndio tukurupuke kutafuta chombo cha maana. Kwa ukurupukaji huu hata hicho chombo tutakachopata tutakuja kulia tu! Wahenga walisema'haraka haraka haina baraka!'
      Hivyo utaratibu gani huo utakaofanyika wakupata fedha within 7 days? Sio hapa tunadanganyana jamani? Tunae Kaka wakuenda kumuomba leo kesho akatupa? Hivyo kama taratibu kama hizo zipo kwanini zisifanyike juzi na jana na tukangojea mpaka maafa yametufika?
      VISION is what we lack in Zanzibar. This is our main problem na wala hatutoweza kusonga mbele without having a vision in our minds. Wazanzibari hatujui tunataka nini na tunaelekea wapi. Mpaka lini tutakuwa kazi zetu kuzima moto tu?
      Anyway, tunangojea hivyo videge vibovu vya kukodi kutoka DSM vianze navyo kudondokadondoka na kutuuwa kila mara ili Zanzibar ianze kufikiria kuwa na usafiri madhubuti wa anga!
      I am really looking forward to that day when Wizara ya Fedha itaambiwa kuandaa utaratibu wa kupata fedha ndani ya wiki moja kwaajili ya kununua ndege mpya ya abiria!

      Delete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.