Habari za Punde

Kuna Mapungufu ya Sera na Sheria za Mazingira - Waziri Ferej

Na Mwantanga Ame
MAPUGUFU ya Sera na sheria zinazosimamia mazingira zimeonekana kuwa na mapungufu jambo ambalo limekuwa likisababisha kuwapo kwa uharibifu wa mazingira katika miradi ya maendeleo inayohusu Barabara na ujenzi wa hoteli.

Hayo yameelezwa jana na Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Fatma Alhabib Ferej, wakati akijibu suala la Mwakilishi wa Jimbo la Mtambile Mohammed Haji Khalid, aliyetaka kujua ni kwanini kuna miradi inayoharibu mazingira wakati kukiwa na sheria zipo.

Akijibu suala hilo Waziri huyo alisma ni kweli kumekuwa na tatizo hilo lakini linatokana na sera na sheria iliopo ya usimamizi wa mazingira katika miradi ya barabara na mahoteli kuwa na mapungufu na inahitaji kufanyiwa marekebisho.

Alisema hivi sasa Wizara hiyo imekuwa ikiifanyia mapitio sheria na sera hiyo ambayo itaweza kutoa adhabu kubwa na kifungo kwa watu ambao watabainika kuharibu mazingira.

Alisema hadi sasa jumla ya miradi 15, ya bara bara na miradi 231 ya hoteli ambapo 12 inayohusu ujenzi wa barabara imefanyiwa tathmini za athari za kimazingira.

Kuhusu miradi ya hoteli alisema miradi 14 kati ya 50 ndio iliyofanyiwa tathmini juu ya athari hizo huku kati ya miradi hiyo 14 nayo imeshafanyiwa kazi hiyo.

Alisema sababu zinazojitokeza kuwapo kwa mambo hayo ni pamoja na kuwapo kwa mwamko mdogo wa wawekezaji katika miradi ya maendeleo ikiwemo ile inayotokana na misaada ambayo huwa ni vigumu kuzingatiwa suala la mazingira.

Aidha alisema pia tatizo hilo limekuwa likichangiwa kuwapo kwa ushirikiano mdogo katika taasisi zinazohusika na Miundombinu na upungufu wa nyezo za ukaguzi.

Alisema kwa mwaka wa fedha uliopita taasisi hiyo, imeweza kukusanya jumla ya shilingi 5,970,000 ikiwa ni sawa na asilimia 120 kwa makadirio iliyojiwekewa mwaka 2011/2012 hatua ambayo imefanya kuvuka lengo kwa asilimia zaidi ya 20.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.