WATOTO katika kijiji cha SOS, mjini Zanzibar
wameshiriki katika chakula cha futari na
mke wa rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza
la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, katika kijiji chao Mombasa
mjini Zanzibar.
Mama Mwanamwema, alishiriki katika chakula hicho juzi usiku
akiwa pamoja na mama Asha Suleiman Iddi, pamoja na Umoja wa wake wa Viongozi na
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib Abdalla Mwinyi Khamis.
Akitoa shukurani zake Mkurugenzi wa kijiji hicho Suleiman
Mahmoud Jabir, alisema wamefurahika na hatua ya Mama Shein na viongozi wengine
wa Zanzibar,
kwa kujali watoto yatima kuwa nao ni sehemu jamii inayohitaji kupata vitu
vizuri ndani ya mwezi huu wa ramadhani.
Alisema jamii ya watoto yatima inapaswa kuangaliwa katika
haki sawa na watoto wengine na kijiji chake kitahakikisha wanashirikiana na
serikali kuona wanapata mahitaji yao
ya lazima ikiwemo haki ya kula na kuishi vizuri.
Mkurugenzi huyo aliipongeza serikali kwa kuendelea kuwajali
watoto yatima wanaoishi ndani ya kijiji hicho kwa kuwapatia misaada mbali mbali
ndani ya mwezi mtukufu wa ramadhani na baada ya mfungo huo.
Mkurugenzi huyo aliahidi kuendelea kushirikiana na serikali
kila pale itaopohitajika kutoa msaada wao.
Hata hivyo, Mkurugenzi huyo alitoa pole kwa wananchi wa Zanzibar waliopatwa na
msiba na waliojeruhiwa katika ajali ya kuzama meli ya Mv. Skagit.
Wakati huo huo, Mama
Mwanamwema Shein, jana jioni alitarajiwa kula chakula cha pamoja na
watoto yatima wanaoishi katika nyumba ya kulelea watoto ya Mazizini.
Afuturia => Afutarisha
ReplyDeleteAssalamu Alaikum.
ReplyDeleteMkuu wa Mkoa Abdalla Myinyi Khamis hapo sio mahala
pa kuweko wewe inakuwaje ujichanganye na wanawake.
Viongozi mna matatatizo ya kusahau au kudhara maamrisho
ya Alla ambae ametuwekea mipaka kwa kila jambo na si
kuendeleza sissa tu na kusahau dini yetu inatuambia nini
hii ni dalili ya kuwa hatuifahamu dini yetu kisawa sawa
Wabillahi Tawfyq
Huyu mzee kwa kweli anatakiwa apumzike tena!...ni kwa vile hakuna mtu wa kuchukua nafasi yake, kwani inasemekana amesomea fani ambayo hakuna Mzenji aliyenayo, ila vinginevyo ameshasaidia vya kutosha!
ReplyDeleteKwani jamani huyu ni Abdalla Mwinyi Khamis au Idarous?
Shukran Mr Muhsin kwa tanbihi ya lugha. Tumeiweka sawa
ReplyDelete