Habari za Punde

Mama Mwanamwema Shein Afutarisha Watoto wa Kijiji cha SOS Mombasa Zanzibar.

Na Mwantanga Ame

WATOTO katika kijiji cha SOS, mjini Zanzibar wameshiriki katika chakula cha futari  na mke wa rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, katika kijiji chao Mombasa mjini Zanzibar.

Mama Mwanamwema, alishiriki katika chakula hicho juzi usiku akiwa pamoja na mama Asha Suleiman Iddi, pamoja na Umoja wa wake wa Viongozi na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib Abdalla Mwinyi Khamis.

Akitoa shukurani zake Mkurugenzi wa kijiji hicho Suleiman Mahmoud Jabir, alisema wamefurahika na hatua ya Mama Shein na viongozi wengine wa Zanzibar, kwa kujali watoto yatima kuwa nao ni sehemu jamii inayohitaji kupata vitu vizuri ndani ya mwezi huu wa ramadhani.

Alisema jamii ya watoto yatima inapaswa kuangaliwa katika haki sawa na watoto wengine na kijiji chake kitahakikisha wanashirikiana na serikali kuona wanapata mahitaji yao ya lazima ikiwemo haki ya kula na kuishi vizuri.

Mkurugenzi huyo aliipongeza serikali kwa kuendelea kuwajali watoto yatima wanaoishi ndani ya kijiji hicho kwa kuwapatia misaada mbali mbali ndani ya mwezi mtukufu wa ramadhani na baada ya mfungo huo.

Mkurugenzi huyo aliahidi kuendelea kushirikiana na serikali kila pale itaopohitajika kutoa msaada wao.

Hata hivyo, Mkurugenzi huyo alitoa pole kwa wananchi wa Zanzibar waliopatwa na msiba na waliojeruhiwa katika ajali ya kuzama meli ya Mv. Skagit.

Wakati huo huo, Mama  Mwanamwema Shein, jana jioni alitarajiwa kula chakula cha pamoja na watoto yatima wanaoishi katika nyumba ya kulelea watoto ya Mazizini.


4 comments:

  1. Assalamu Alaikum.
    Mkuu wa Mkoa Abdalla Myinyi Khamis hapo sio mahala
    pa kuweko wewe inakuwaje ujichanganye na wanawake.
    Viongozi mna matatatizo ya kusahau au kudhara maamrisho
    ya Alla ambae ametuwekea mipaka kwa kila jambo na si
    kuendeleza sissa tu na kusahau dini yetu inatuambia nini
    hii ni dalili ya kuwa hatuifahamu dini yetu kisawa sawa

    Wabillahi Tawfyq

    ReplyDelete
  2. Huyu mzee kwa kweli anatakiwa apumzike tena!...ni kwa vile hakuna mtu wa kuchukua nafasi yake, kwani inasemekana amesomea fani ambayo hakuna Mzenji aliyenayo, ila vinginevyo ameshasaidia vya kutosha!

    Kwani jamani huyu ni Abdalla Mwinyi Khamis au Idarous?

    ReplyDelete
  3. Shukran Mr Muhsin kwa tanbihi ya lugha. Tumeiweka sawa

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.