Habari za Punde

Mwanza, Moro vitani fainali Copa Coca Cola


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
TIMU za vijana (U-17) za Mkoa wa Mwanza na Morogoro, leo zinapambana kuwania taji la michuano ya Copa Coca-Cola 2012, mchezo utakaopigwa kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam kuanza saa 9:00 alasiri.

Mwanza ilikata tiketi ya kucheza fainali baada ya kuifunga Temeke mabao 3-1, wakati Morogoro iliitupa nje Tanga kwenye nusu fainali kwa ushindi wa mabao 3-1 pia.

Mechi ya kutafuta mshindi wa tatu kati ya Temeke na Tanga itachezwa kwenye uwanja huo huo kuanzia saa 5:00 asubuhi.

Mashindano ya Copa Coca-Cola 2012 yalianza Juni 24 mwaka huu yakishirikisha mikoa 28 ya Tanzania Bara na Zanzibar.





No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.