Na Mwanajuma Mmanga
JESHI la Polisi kitengo cha kupambana na Dawa za Kulevya kwa kushirikiana na Polisi Jamii kimefanikiwa kumtia mbaroni mwanamke unaoaminika kuwa ni dawa za kulevya.
Akizungumza na mwandishi wa habari, ofisini kwake Naibu Mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai Makao Makuu ya Polisi, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Yussuf Kombo, alimtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Zarina Suleiman Mussa, (31) mkaazi wa Ilala, jijini Dar es Salaam.
Alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa Juni 30 mwaka huu, majira ya 8:25 mchana katika kiwanja cha ndege cha Zanzibar akijianda kusafiri kwa ndege ya Ethiopian Airline kuelekea nchini Ufaransa.
Kamishna huyo alisema dada huyo aliyebambwa na unga alikuwa na hati ya kusafitia nambari AB.449275, iliyotolewa jijini Dar es Salaam Januari 20 mwaka jana.
Alisema uchunguzi wa awali unaonesha kuwa unga aliokamatwa nao ni heroine.
Alifahamisha kuwa mtuhumiwa huyo ambaye alikuwa amefikia maeneo ya Maisara, alipokamatwa na unga huo akiwa ameuhifadhi kwenye plastiki na kuuingiza kwenye begi lake la kusafirishia na baadae kuufunga kwa vitu ambavyo haviwezi kunaswa na mashine ya X ray, wala kunuswa na mbwa.
Naibu Mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai aliwataka wananchi kulisaidia jeshi la polisi kutoa taarifa za aina kama hiyo kwa lengo la kudhibiti uingizwaji na usafirishaji wa dawa hizo.
Kwa upande wake Mkuu wa kitengo hicho Mratibu Mwandamizi wa polisi, Mkadam Khamis, alisema kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa akipeleka dawa hizo nje ya Tanzania, lakini kukamatwa kwake Zanzibar kunaweza kuvunja hadhi na heshima ya visiwa hivi.
Alisema hii ni mara ya pili kitengo hicho kukamata kiwango kikubwa cha unga ya dawa ya kulevya kwa uwanja wa ndege wa Zanzibar kwa mwaka huu.
Dkt. Mwinyi Aagiza Elimu ya Branding Kuwafikia Watanzania Wote
-
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dkt.Hussein Ali
Mwinyi, amesema kuwa katika kipindi hiki cha mabadiliko, Serikali
inaendelea kufany...
8 hours ago
No comments:
Post a Comment