Na Mwantanga Ame
SERIKALI ya Zanzibar, imewataka wananchi kisiwani Pemba kuwa tayari kuwapo kwa mabadiliko katika uwanja wa ndege wa Karume, ikiwa ni hatua itayochukuliwa na serikali kuimarisha huduma za uwanja huo.
Naibu Waziri wa Wizara Miundombinu na Mawasiliano, Issa Usi Haji Gavu, aliyasema hayo jana wakati akijibu suala la Mwakilishi wa viti vya wanawake, Shadya Mohammed Suleiman, aliyetaka kujua ni hatua zipi serikali inaziandaa kuufanyia matengenezo uwanja huo.
Alisema hivi sasa Wizara hiyo imo katika utaratibu wa kukamilisha mipango ya ukarabati wa uwanja huo ili wananchi waweze kufaidika na huduma zake.
Alisema Wizara tayari walishakubaliana na Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB), ili kupata fedha za kuanza kwa ujenzi.
Omar Ali Sheikh, nae alihoji ni kwanini ndani ya kipindi cha katika Wizara hiyo kuna maelezo ya kukiimarisha kiwanja hicho, lakini hakuna kinachofanyika na ni sababu zipi zilizofanya matengenezo hayo yasifanyike wakati kuna fedha zinazotengwa.
Akijibu suala la Mwakilishi Omar Ali Shehe, alietaka kujua sababu za wizara kushindwa kuufanyia matengeno uwanja huo, Naibu Waziri huyo alisema hilo linaweza kuchangiwa kutokana na Wizara hiyo hivi sasa imo katika kufanya uchambuzi yakinifu kuweza kuufanyia mabadiliko uwanja huo.
Alisema suala la kutengwa bajeti ilikuwa linafanyika lakini kumekuwa kukijitokeza mahitaji mengine kutokana na kusubiri matokeo ya uchambuzi huo.
Nae Asha Bakari ambae aliktaka kujua ni kwa nini jengo hilo hivi sasa halina uzio, Naibu Waziri huyo alisema ni kweli hilo lipo, lakini limechangiwa na bajeti ndogo.
No comments:
Post a Comment