Na Hafsa Golo
KAMPUNI ya Salim Construction Co Limited imesema ifikapo mwezi Septemba 2012, itaikabidhisha rasmi skuli ya Tumekuja kwa wizara ya elimu kwa kuwanza kutumika.
Ahadi hiyo imetolewa na Muangalizi na Meneja wa Kampuni hiyo, Khuzema S.Adamjee wakati alipotembelewa na uongozi wa wizara ya elimu skulini hapo kutaka kujua hatua za ukarabati zilizofikiwa katika skuli ya Tumekuja na Forodhani.
Alisema kuwa ukarabati wa skuli hiyo ambao ulitumia asilimia 87 za mbao na asilimia 75 za vifaa vipya kutokana na uchakavu wa baadhi ya vifaa hivyo.
Aidha alisema pamoja na changamoto zilizojitokeza katika ukarabati huo kilichozingatiwa zaidi utekelezaji wa maagizo ya Mji Mkongwe ili ujenzi huo usikiuke kumbukumbu za awali jambo ambalo lingeweza kuondosha historia ya jengo hilo.
"Skuli hii awali mbao zilizotumika ni msaji, ambazo zani za asili na takriba nyingi zimeoza lakini kuna vibande vilivyokuwa vizima tumevitumia na visivyofaa tumetumia mbao za mninga ila madirisha tumetimia yaleyale, na mahamam yapo vile vile na vitu vya zamani vimebaki"alisema
Nae Mhandisi wa wizara hiyo, Maulid Hassan alisema jumla ya pesa zilizotumika ni shilingi 531,622,491 kwa skuli ya Tumekuja shilingi 650,771,530 kwa skuli ya Forodhani.
Alisema kwa upande wa skuli ya tumekuja ambayo inatarajiwa kufunguliwa hivi karibuni itakuwa na madarasa zaidi ya 10. na chumba kimoja cha lebo wakati awali ilikuwa haipo na vyoo 30,pamoja na stafu za walimu.
Na kwa upande wa skuli ya Forodhani alisema kutokana na ukubwa wa vyumba wametowa lebo 3 ikiwemo ya phy.biologia,na chemistry na madarasa kumi na saba ya kusomea.
"Kutakuwa lebo3. chumba cha computer,madarasa yasiopungwa 17,ukarabati ni mgumu hasa tikizingatia nyezo tunazitumia kwa ajili ya kurejesha uasili wake wa mwazo,kwani walitumia udongo na chokaa,alisema
Kwa upande wa waziri wa elimu na mafunzo ya amali Ali Juma Shamhuna alisema kuwa kumalizika kwa skuli hiyo kutaondosha wimbi la wanafunzi kusongamana katika madarasa.
Pia alisema skuli hizo zitaweza kusaidia kupunguza changamoto ya lebo za masomo ya sayansi ambazo zinatukabili kwa muda mrefu/
Waziri Shamhuna alisema uamuzi wa kuyakarabati majengo ya skuli, ni hatua moja ya kuimarisha maendeleo ya elimu kwani kuachwa kuendelea kubomoka ni kupunguza majengo ya skuli na changamoto zisizo za ulazima.
No comments:
Post a Comment