Habari za Punde

Utoaji wa Maoni ya Katiba ya Tanzania Wilaya ya Kusini Jambiani Paje na Bwejuu.

Wananchi wa Kijiji cha Jambiani wakiwa katika utaratibu wa kupanga mstari ili kuweza kutowa maoni yao kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilipofika Kijijini hapo kukusanya maoni ya Wananchi wa Jambiani
 Wananchi wa Kijiji cha Jambiani wakiwa katika utaratibu wa kupanga mstari ili kuweza kutowa maoni yao kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilipofika Kijijini hapo kukusanya maoni ya Wananchi wa Jambiani katika viwanja vya Skuli ya Jambiani.
 Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba wakikusanya Maoni ya Wananchi wa Kijiji cha Jambiani.
 Mwananchi wa Kijiji cha Jambiani akiwasilisha maoni yake kwa njia ya Barua kwa Tume.
 wananchi wa kijiji cha jambiani wakisubi zao yao nao waweze kutowa maoni yao kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Tanzania, ilipofika katika viwanja vya Skuli ya Wilaya ya Kusini Unguja.
 Wazee wa Jambiani wakiwa nje ya  Ukumbi wa kutolea maoni ya Marekebisho ya Katiba  wakibadilishana mawazo baada ya kutumia haki yao kisheria ya kutowa maoni yao juu ya uundaji wa Katiba Mpya ya Tanzania
 Vijana wa Kijiji cha Jambiani wakisoma baadhi ya Vifungu vya Katiba ya Zamani kabla ya kuingia katika ukumbi wa kutoa maoni yao katika skuli ya Jambiani.
 Wananchi wa Shehia za Paje na Bwejuu wakiwa katika viwanja vya mpira bwejuu wakisikiliza maoni ya wananchi wanayoyatowa mbele ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba Tanzania.








No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.