Habari za Punde

Wakimbizi Wapokelewa Nyumbani Leo


Watanzania waliokuwa wakimbizi katika kambi ya Mogadishu wakielekea kupanda mabasi maalum yaliyoandaliwa na Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa baada ya kuwasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume jana

Watoto ambao kwa sasa ni Raia wa Somalia wakiwa na wazazi wao Raia wa Tanzania waliokuwa wakimbizi nchini Somalia wakisubiri taratibu za Uhamiaji katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume jana baada ya kuwasili wakitokea Mogadishu na ndege ya Umoja wa Mataifa chini uangalizi wa UNHCR
Baadhi ya akinamama Raia wa Somalia ambao wameolewa na Watanzania waliokuwa ukimbizini Mogadishu wakifurahia jambo walipowasili uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume,hapa walikuwa wakisubiri taratibu za Uhamiaji


Baadhi ya Watanzania waliokimbilia Mogadishu mwaka 2001 wakiwa katika Ofisi ya Uhamiaji Zanzibar jana. Wa kwanza ni Mohammed Adam(38) akiwa amembeba mwanawe mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume,wanaotazama kamera ni baadhi ya wake wa Watanzania hao ambao ni raia wa Somalia waliowasili jana wakitokea Mogadishu Somalia na ndege ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia huduma za kibinadamu

Baadhi ya Wanzania 38 waliokuwa wakimbizi Jijini Mogadishu wakielekea sehemu ya mapokezi mara baada ya kushuka katika ndege la Umoja wa Mataifa iliyowaleta nyumbani wakiwa na wake zao walioa nchini Somalia baada ya kuishi huko kwa miaka 11,walikimbia vurugu za Januari 26/27 mwaka 2001

(Picha na Juma Mohammed,MAELEZO Zanzibar)

1 comment:

  1. Karibuni nyumbani wandugu, lkn na hapa pia si shwari sana kwani UWAMSHO tayari wanataka kuturejesha kule kule tulikotoka!

    Labda mtatusaidia kuwaelimisha maana 'adhabu ya kaburi aijuae maiti'..huenda nyinyi wakawaelewa.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.