Habari za Punde

Wananchi Wakiwa katika Viwanja vya Maisara Kutambua Miili ya Jamaa Zao.

Watalii kutoka Nchini Italia wakiwa katika viwanja vya maisara katika zoezi la klutambua miili ya Watu waliofariki kastika ajali ya boto ambayo walikuwemo Watalii na kati yao mmoja amefariki katika ajali hiyo.

Mzee Ali Hassan Mwinyi akiwasili katika viwanja vya maisara ili kutowa pole kwa Wananchi waliofiwa na jamaa zao.
Rais Mstaafu  Mhe Ali Hassan Mwinyi akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali waliofika katika eneo hilo maalum kwa ajili ya kuwatambua maiti wa ajali ya boti.
Rais Mstaafu wa Tanzania Mhe Ali Hassan Mwinyi akimsikiliza Dk. Marijani , alipofika katika viwanja vya maisara kutowa pole na kuangalia utaratibu wa kuwatambua marehemu na jamaa zao.



Jamaa  wa Marehemu Sauda Juma ambaye ni Raia wa Rwanda  ambaye amafariki katika ajali hiyo, wakisubiri maiti yao ili kwenda kuzikwa.
Mkurugenzi Biashara wa Kampuni ya Zantel  Zanzibar Mohammed Mussa,akikabidhi  msaada wa sada Katibu Mtendaji wa Wakfu Abdalla Talib,kwa  maiti wa ajali ya boti, makabidhiano hayo yamefanyika viwanja vya maisara,
Wafanyakazi wa kampuni ya simu ya Zantel wakitowa huduma ya maji na biskuti kwa Wananchi wanaofika kutambua miili ya jamaa zao na watoa huduma katika kituo hicho.
Mmoja wa Abiria aliyenusurika katika ajali hiyo Tatu Piela , akipata  kikombe cha uji kutoka kwa wasamaria waliofika katika viwanja vya maisara , ambaye na mweji wa Isaka Shinyanga, amepoteza  mtoto Said Jumanne mwenye umri wa miezi 9 wake, akisubiri kukabidhiwa maiyi yake kwa ajili ya kwenda kuzika.  

Waheshimiwa Mawaziri na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Mashehe wakiwa katika viwanja vya maisara kuwafariji jamaana ndugu waliofiwa na jamaa zao.
Maofisa wa  Wakfu na Mali ya Amana wakiandaa sanda kwa ajili ya kutowa kwa jamaa wa marehemu ili kuzikia  iliotolewa na Serekali kwa Wananchi waliofariki katika ajali hiyo. na kusaliwa katika viwanja hivyo.  

Maofisa wa Ubalozi wa  Scandinavia wakiwa katika viwanja vya Maisara kukagua mwili wa mmoja wa Mtalii aliofariki katika ajali hiyo.
Wananchi  wakikagua maiti ili kutambua maiti za jamaa zao katika viwanja vya maisara ambavyo vimetengwa kwa ajili kufikisha maiti wanaookolewa katika ajali hiyo.
Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Asha Bakari Makame, akizungumza na waandishi wa habari  alipofika katika viwanja  vya maisara  alipofika kutoa pole kwa wananchi waliofiwa na jamaa zao.  

Meneja wa Kitengo cha Data  katika Wizara ya Afya Zanzibar Mohammed Habibu, akitowa idadi ya wananchi waliopokelewa na  majeruhi na wale waliofariki, kutokana na ajali hiyo, akiwa katika kituo cha kupokelea maiti maisara.
Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu Hamad Masoud akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali waliofika katika viwanja vya maisara kulikotengwa kwa ajili ya kuwatambua marehemu wa ajali ya boti iliotokea jana 18-7-2012 katika bahari ya Zanzibar maeneo ya Chumbe,
Naibu Amir, Azan Hamdani, akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya maisara.
 Jamaa wa mmoja wa marehemu wa ajali ya Boti akiwa na simanzi ya kuondokewa na jamaa yake katika tukio la ajali hiyo, baada ya kuitambua maiti ya jamaa yake iliopelekwa katika viwanja vya maisara.
 Baadhi ya Wanandugu wakiwa katika foleni kusubiri kutambua miili ya Ndugu zao waliopata ajali ya kuzama kwa boti ya Kampuni ya SeaGull.jana katika  bahari ya Zanzibar.
Wananchi wakiwa katika viwanja vya mpira Mairasa kusubiri kutambua miili ya jamaa zao.

Wananchi wakiwa katika Ufukwe wa bahari ya Kizingo wakiangalia  kama kutakuwa na miili kuangukia katika ufukwe huo ili kuwatambua jamaa zao.

1 comment:

  1. Mola awape moyo wa subira wafiwa wote na waliofikwa na msiba huu. Ahsante brother Mapara kwa kuendelea kutupatia yanayoendelea hasa sisi tulio mbali na nyumbani.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.