WIZARA ya Habari Utamaduni, Utalii na Michezo imesema imeanza kuwapatia mafunzo wafanyakazi wa ZBC Redio, na ZBC TV, ikiwa ni hatua ya kuwaweka tayari kumudu mfumo wa matumizi ya digitali.
Waziri wa Wizara hiyo, Said Ali Mbarouk, aliyasema hayo jana wakati akijibu suala la Mwakilishi wa Jimbo la Micheweni Subeit Khamis Faki, aliyetaka kujua kama Wizara hiyo tayari imeshawaandaa wafanyakazi wa taasisi hiyo ili kumudu kuutumia vyema mfumo huo wa digitali.
Waziri huyo alisema wizara hiyo kwa kufahamu umuhimu wa suala hilo tayari hivi sasa imeanza kuwapatia mafunzo wafanyakazi hao yanayoendeshwa na Mtaalamu kutoka nchini Ujerumani.
Alisema dhamira ya kutoa mafunzo hayo ni kuona wafanyakazi hao wanakuwa katika hali nzuri kuendesha matangazo yao kwa mujibu wa mabadiliko ya kisasa.
Alisema mafunzo hayo pia yanatarajiwa kutolewa tena na wataalamu kutoka katika Shirika la Utangazaji la Duch walle ambayo yatafanyika mwezi Agosti.
Waziri huyo pia alieleza serikali haitaweza kuondoa misamaha ya kodi katika vifaa vyenye mfumo wa digitali kwa vile wataopewa msamaha huo bado watakuwa wanafanya biashara jambo ambalo linaweza likasababisha wananchi wasifaidike na mpango huo.
Akijibu suala la msingi la Mwakilishi wa Matemwe, Abdi Mosi Kombo, aliyetaka kujua kama Wizara hiyo imeshawaelimisha wananchi wake wa Unguja na Pemba juu ya mfumo huo, Naibu wa Wizara hiyo Bihindi Juma Hamad, alisema tayari kazi hiyo imefanyika kuanzia mwaka 2006 kwa kutumia njia mbali mbali.
Alisema hivi sasa Wizara hiyo kupitia Tume ya Utangazaji Zanzibar, inakusudia kuendesha kampeni Maalum ya Umma ambayo itawashirikisha wananchi wanaoishi mijini na vijijini ambayo inatarajiwa kuanza kufanyika 2012/2013.
WANANCHI WAASWA KUTUMIA NAMBA YA MALIPO WANAPOLIPIA HUDUMA ZA SERIK
-
Afisa Mwandamizi kutoka Idara ya Usimamizi wa Mifumo ya Fedha na TEHAMA wa
Wizara ya Fedha, Bw. Charles Maganga (kulia), akitoa maelezo kuhusu umuhimu
wa...
19 minutes ago
No comments:
Post a Comment