Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Uongozi wa Benki ya Posta Tanzania Tawi la Zanzibar uliofika Ofisini kwake kutoa mchango wa Maafa kutokana na ajali ya Meli ya M.V.Skagit na Harakati za Sensa Nchini Tanzania.
Meneja wa Benki ya Posta Tanzania Tawi la Zanzibar Bwana Justin Stephen Justin Nandende akimkabidhi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Mchango wa Shilingi milioni Nne
{ 4,000,000/- }. Kati ya hizo Shilingi Milioni mbili kwa ajili ya Mfuko wa Maafa Zanzibar na Shilingi MilioniMbili kwa ajili ya harakati za Sensa.
Hafla hiyo imefanyika Ofisini kwa Balozi Seif Vuga Mjini Zanzibar.
Menaja wa Benki ya Posta Tanzania Tawi la Zanzibar Bwa. Justin Stephen Justin Nandonde akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Uongozi wa Benki ya Posta Tanzania Tawi la Zanzibar ukisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar kuwasilisha mchango kwa ajili ya mfuko wa Maafa na harakati za Sensa ya Watu nan Makazi Tanzania.
Picha na Saleh Masoud Mahmoud – OMPR- ZNZ
Na Othman Khamis Ame
Benki ya Posta Tanzania itaendelea kuunga mkono harakati za Maendeleo ya Kijamii na Serikali katika kuona ustawi wa Wananchi unaimarika siku hadi siku hapa Nchini.
Kauli hiyo imetolewa na Meneja wa Benki ya Posta Tanzania Tawi la Zanzibar Bw. Justin Stephen Justin Nandonde wakati akiwasilisha Mchango wa shilingi Milioni Nne { 4,000,000/- } kwa ajili ya mfuko wa Maafa Zanzibar na Shughuli za Sensa ya Watu na Makazi Tanzania.
Bwana Justin Nandonde aliwasilisha Mchango huo kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Meneja wa Benki hiyo ya Posta Tanzania Tawi la Zanzibar alimueleza Balozi Seif kwamba Taasisi yao ilikuwa imeshajiandaa kuchangia harakati za Sensa Nchini lakini wakati huo huo ikajikuta inapokea Taarifa ya kuzama kwa Meli ya M.V. Skagit Tarahe 17/7/2012 .
Bwana Nandende alisema hali hiyo ilipelekea Uongozi wa Benki yake kufikiria kutoa mchango kwa masuala yote mawili ambayo tayati Benki hiyo inahusika nayo kwa vile Taasisi hiyo ni Mshirika wa karibu na Jamii Nchini.
“ Tulifikia maamuzi ya kutoa hichi hichi kidogo tulichokipata cha Shilingi Milioni 2,000,000/- kwa mfuko wa Maafa Zanzibar na Shilingi Milioni 2,000,000/- kwa harakati za Sensa Nchini”.Alifafanuwa Bwana Nandonde.
Akipokea Mchango huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliupongeza Uongozi wa Benki hiyo ya Posta Tanzania kwa uwamuzi wake iliyofikia wa wa kutoa mchango huo ambao utasaidia katika maeneo yote mawili.
Balozi Seif alisema amefarajiwa kuona Uongozi wa Benki hiyo umeguswa na tukio la Maafa ya kuzama kwa Meli ya M.V. Skagit iliyosababisha watu 142 kufariki Dunia na wengine 146 waliokolewa hai kati ya watu 192 walioripotiwa kusafiri na Meli hiyo kutokea Dar es salaam kuelekea Zanzibar.
Akigusia suala la Sensa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akiwa pia Mwenyekiti Mwenza wa Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa Tanzania Balozi Seif alisema zoezi la kuhesabu Watu si geni Nchini lakini linaonekana baadhi ya Watu kuliingiza katika Siasa kwa kisingizio cha Dini.
Hata hivyo Balozi Seif alisema Taarifa zilizopatikana kutoka Mikoa mbali mbali Nchini Bara na Zanzibar tokea kuanza kwa zoezi la kuhesabu Watu zinaonyesha maendeleo mazuri ya zoezi hilo.
Balozi Seif alisema hatua hiyo imelitia moyo Taifa kutokana na hali ya kabla kukumbwa na wimbi la kususia kushiriki zoezi la sensa lililokuwa likiendeshwa na baadhi ya Viongozi wa Kidini.
Alifahamisha kwamba lengo la Sensa ni Uchumi na Mipango ya Maendeleo ya Taifa kwa vile huduma zitakazotolewa baada ya uelewa wa idadi ya Watu na Maeneo zitamuhusu kila mwana jamii.
“ Tanzania inahitaji kujua Takwimu za mambo yake yote iwe ya shughuli za Elimu, Afya, Miundombinu au miradi ya Jamii”. Alisisitiza Balozi Seif.
Alitanabahisha kwamba zoezi la Sensa ya watu na makazi halihusiki kabisa na Dini au Siasa.
No comments:
Post a Comment