Habari za Punde

DK.Kihiyo atishia afya za wageni Zanzibar.Daktari’ adaiwa kutumia vyeti vya marehemu

Na Mwandishi Wetu (Dotto Mwaibale) 0712-727062
 
Mtu mmoja anayejitambulisha kama daktari na mmiliki wa kiliniki moja ya binafsi inayojihusisha na kutoa huduma ya afya kwa watalii visiwani Zanzibar anadaiwa hana taaluma hiyo bali anatumia vyeti vya daktari aliyefariki mwaka, 2000.

Daktari anayedaiwa kutumia vyeti vya marehema ametajwa kwa jina moja la Yusuf mzaliwa wa mkoa wa Mtwara wakati marehemu (mwenye vyeti) ametajwa kwa jina la Dk.Haroun Ally aliyekuwa akifanyakazi katika hospitali ya serikali ya Sokoine iliyopo mkoani humo.

Taarifa zaidi zinasema Yusuf amekuwa akijinasibu kuwa alisomea elimu ya utabibu katika chuo cha serikali cha Mtwara Medical Training Centre (MTC) wakati ukweli ni kwamba aliyesoma hapo ni Dk.Haroun Ally,marehemu.

Akijibu swali kuhusu madai hayo mdaiwa (Yusuf) alikana tuhuma hizo na kudai yeye ndiye aliyesomea udaktari katika chuo hicho na kwamba anatumia majina matatu toka akiwa chuoni ambayo ni Haroun Ally Niva, ingawa uongozi wa chuo umekanusha kuwepo mtu anayeitwa Dk.Haroun

Ally Niva bali kumbukumbu zilizopo ni za mtu anayeitwa Dk.Haroun Ally ambaye sasa ni marehemu.

Mkuu wa chuo cha MTC Dismas Mlelwa ambaye wakati Dk.Haroun (marehemu) anasomea udakitari chuoni hapo miaka ya themanini yeye akiwa mwalimu wa kawaida alisema anayemtambua ni Dk.Haroun aliyefariki na si vinginevyo.

“kumbukumbu zetu zinaonesha Haroun Ally alikuwa mwanafunzi wetu hapa chuoni hatuna mtu mwingine zaidi ya huyo” alisisitiza Dk.Mlelwa alipohojiana na mwandishi wa hahabri hizi.

Daktari anayetuhumiwa , alikiri kumiliki kliniki visiwani Zanzibar inayotibu watalii toka nchi mbalimbali na kwamba chanzo cha kuitwa yeye si daktari ni ugomvi kati yake na baadhi ya wateja wake wa kigeni ambao alidai walimzushia kuwa yeye ni daktari feki na kuchapisha habari nyingi katika mtandao wa Twiter na Facebook.

Raia wawili wa kigeni walilalamikia Wizara ya Afya ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuhusu daktari huyo wakidai hana taaluma ya udaktari na amekuwa akitoza gharama kubwa ni Ron Benamotz na Inguid Falkum wote raia wa Norway ambao wanadai kutibiwa na Dk.Haroun kati ya tarehe 22-10-2011 ambapo alilipa dola 189 sawa na sh.299, 500 za kitanzania.

Raia hao walilalamika katika mtandao wa Twitter,Facebook na Trip Adiviser kuwa watalii wenzao wengi walitambua kiliniki ya Dk.Haroun kwa kusoma katika tovuti yake ya www.almanatours.com daktari huyo anatibu watalii na ana vifaa vya kutosha zikiwemo Helkopta za uokoji, magari ya kukimbiza wagonjwa na boti ziendazo kasi, huku vitu hivyo hana.

Hata hivyo Dk.Haroun ‘aliyehai’ alikiri kuwa hana vifaa hivyo bali huvikodi toka kwa watu binafsi wanaomiliki vifaa hivyo.

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kupitia ofisa mmoja wa ngazi za juu anayesimamia masuala ya afya alikiri kuwepo kwa madai hayo na kwamba yanafafanyiwa uchunguzi na ikibainika mtu huyo anafanya mambo hayo hatua za kisheria zitachukuliwa.

“Kwa sasa sitaki utaje jina langu gazetini nitaharibu uchunguzi wa suala hili, kweli yapo madai kama hayo na tukibaini kweli hayo yanafanyika tutachukua hatua” alisema ofisa huyo.

Msaidizi wa Mrajis wa Bodi ya Hospital binafsi Dr Shaabani Seif Muhamed alisema kuwa kufuatia tuhuma zinazozungumzwa na baadhi ya wananchi juu ya daktari Haroun Ali kwa kuifanyiakazi hiyo bila ya kuwa na taaluma nayo kwa kile kinachodaiwa anatumia cheti kisichokuwa chake hivyo usimamizi wa bodi hiyo haitoweza kufanya maamuzi yoyote kwani hakuna mtu yoyote ikiwa mgeni wala mzaliwa kupeleka malalamiko katika bodi hiyo.

Alisema hayo wakati alipokuwa akizungumza na gazeti hili huko uwanja wa Demokrasia Nje ya Manispaa ya mji wa Zanzibar.

“Huo ni uvumi usio kuwa na uthibitisho kwani mpaka sasa hakuna mgeni hata mmoja alieripoti kwetu wala wananchi ila utasikia tu hiyo hali inazungumzwa lakini haijafika ili tukalifanyia kazi kama bodi”alisema

Mrajisi alisema kuwa bodi yake inamtambua daktari huyo, kwani awali ilimsajili akiwa Clinical Ofice katika kituo cha Afya cha Praivet Kijiji cha Nungwi Almana Mkoa wa kusini Unguja

“Daktari huyu tunamuelewa katika bodi ya Hospitali binafsi na kopi zake zilikuwepo zikiwa na picha yake na jina Lake katika kopi za veti alivyovileta ni la haroun Ali”alisema

Hata hivyo alisema kuwa baada ya kutokeya mzozo kati ya daktari huyo na mmiliki wa jingo la Almana Mmad Shamte, ambalo alikuwa analitumia katika kutoa huduma za afya,alifukuzwa na miliki wa jingo hilo alitoa taarifa kwetu na kama bodi ikawa na uwelewa wa daktari huyo hayupo tena katika kituo hicho.

Sambamba na hayo alisema kuwa hivi sasa daktar huyo inasemekana anafanyakazi katika mahoteli mbalimbali,jambo ambalo bodi haikuwa na sababu za msingi za kumfatilia zaidi kwani hali hii ni madaktari wengi huitumia katika kukudhi ugumu wa maisha.

“Tunasikia anafanyakazi mahotelini akiwa kama daktari na hili daktari wengi hufanyakazi sehemu hizo kwa kujipatia riski kutokana na hali ya maisha”alisema



No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.