Haji
Nassor na Asha Abdallah, ZJMMC Pemba
KIJANA
Khamis Ali Othuman (32) Mkaazi wa Muharitani Wilaya Chake chake Pemba, amepandishiwa katika kizimba cha Mahakama ya
Wilaya hiyo kwa tuhuma za kumtorosha mtoto wa kiume (7) kwa lengo la kumuingilia kinyume na maumbile.
Akisomewa tuhuma hizo mbele ya Hakimu wa
Mahakama hiyo Omar Hamza Mcha, na Mwendesha Mashitaka Gongo Shaaban Gongo,
alidai kuwa Augosti, 19 mwaka huu, majira ya saa 11:00 jioni huko Skuli ya
Michakaini mtuhumiwa huyo, aligundulika
akiwa na mtoto bila ya ruhusa ya wazazi wake.
Mwendesha Mashitaka huyo alidai kuwa
mtuhumiwa huyo alifanya kosa hilo ambalo ni kosa
kwa mujibu kifungu 130 (b) cha sheria namba 6, ya mwaka 2004 ya Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar.
Aidha Mwendesha Mashitaka huyo alidai kuwa
upelelezi wa kosa hilo
bado huajakamilika na kuiomba Mahakama kulipangia siku nyengine ili kuendelea kusilikizwa wakati ukiwa upelelezi
umeshakamilika.
Mapema mthumiwa huyo aliiomba Mahakama
kupelekwa hospitali kutokana na afya yake kudhoofu siku hadi siku kutokana na
kipigo alichadai kupata kutoka kwa Polisi jamii wakati alipokutwa katika eneo
la tukio akiwa na mtoto huyo.
Alidai kuwa kwa sasa hawezi kula vizuri
kutokana na kutapika damu, hivyo hawezi kuishi rumande na kuomba apunguziwe
muda wa kuweko huko badala ya wiki mbili iwe wiki moja na hasa kwa vile ni hivi
karibuni alitoka jela.
‘’Mheshimiwa Hakimu, hali yangu mbaya sana, maana nimerudi jela
hivi karibuni, hivyo kutokana na kipigo cha Polisi Jamii nilichokipata naomba
nipewe dhamana na kupelekwa hospitali kwa matibabu’’, alidai Mtuhumiwa huyo.
Hata hivyo Mtuhumiwa huyo ameomba kupatiwa
dhamana, ombi ambalo lilipingwa na Mwendesha Mashitaka kwa madai kuwa, endapo mtuhumiwa
atapewa dhamana anaweza kudhuriwa na walalamikaji wa shauri hilo kutokana na ukubwa wa kosa lenyewe.
Hakimu wa Mahakama hiyo Omar Hamza Mcha
aliagiza kupelekwa hosptali ili apatiwe matibabu na ameamuru mtuhumiwa huyo
kurejeshwa rumande hadi Septemba 4, mwaka huu na kesi yeke itakapotajwa tena na
siku hiyo dhamana yake itakuwa wazi.
No comments:
Post a Comment