Na Fatuma Kitima, DAR ES SALAAM
RAIS Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Benjamin William Mkapa, amesisitiza kuwa mkataba wa ushirikiano wa kiuchumi kati ya jumuiya ya Ulaya na Afrika (EPA), kuwa hauna tija kwa taifa.
Akizungumza katika hafla ya kusherekea siku ya sekta binafsi (TPSF) jijini Dar es Salaam, Mkapa alisema kuwa mkataba huo wa uchumi hauna maslahi kwa nchi za Afrika Mashariki hasa Tanzania.
Mkapa alisema Jumuiya ya Ulaya zinataka kuondoa kodi nchi za Afrika katika baadhi ya bidhaa na malighafi pamoja na bidhaa zao ziondoe kodi jambo ambalo litaathiri uchumi wa nchi hizo.
Alieleza kuwa kutokana na ugumu wa masharti hayo wamelazimika kujadili suala hilo ili baadae waunganishe mawazo yao.
Alisema Tanzania haipo tayari kusaini mkataba huo kwa kuwa wadau wengi wamekataa na kuufananisha na nyanya. “Sisi tutaendelea kutoa kodi ili kuwezesha viwanda vyetu viendelee”,alisema.
Hata hivyo alisema nchi za Ulaya haziko tayari kuzijengea uwezo wa uchumi nchi za Afrika Mashariki na kuzitaka ziregeze kamba na kuweka sheria laini ili kuweza kupata afueni.
Naye Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Abdallah Kigoda alisema kuwa sekta binafsi zina fursa kubwa kwa serikali katika kushauri mambo mbalimbali pamoja na kuchangia uchumi wa nchi.
Dk. Kigoda alisema kuwa sekta hizo ziko tayari kuongea na umma pamoja na kufanya vikao mara kwa mara.
No comments:
Post a Comment