Habari za Punde

TCRA yawafunda watangazaji, waandaaji vipindi

Na Kunze Mswanyama, DAR ES SALAAM
WATANGAZAJI na waandaaji wa vipindi vya redio televisheni wametakiwa kutumia lugha sahihi zenye staha zinazoendana na maadili na kuzizingatia sheria zanchi.

Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Clement Mshana alieleza hayo jana kwenye semina ya iliyowashirikisha watangazaji na waandaji wa vipindi vya redio na televisheni iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Semina hiyo iliyokuwa na lengo la kuwazindua watendaji hao wa vyombo vya habari ilikuwa na lengo la kuwakumbusha wajibu wao katika matumizi ya lugha sambamba na kuzingatia uzalendo.

Mshana alisema moja ya jukumu kubwa linalowakabili watangazaji na waandaaji wa vipindi ni kuhakikisha wanazingatia maadili jambo ambalo litaondosha kasoro mbali mbali zinazojitokeza hivi sasa katika vyombo hivyo.

Mkurugenzi huyo alisema baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa havina vipindi ambapo kazi yao kubwa ni kupiga mziki muda wote huku wakijua kuwa wasikilizaji wao hawataendelea kwa kusikia muziki tu.

“Kama wewe utakuwa unajua muziki tu hata kimataifa huwezi kusimama na kuzungumzia jambo lolote la kitaifa maana unachofahamu ni aina za muziki tu huku ukiwa na kiwango kidogo cha ufahamu wa masuala mengine kama elimu, utamaduni na uchumi”,alisema.

Aidha Mkurugenzi huyo, alivitaka vyama vya waandishi wa habari kama cha mazingira, UKIMWI kutumia nafasi yao kuwaelekeza na kuwaonya wananchama kila pale matatizo yanapojitokeza.

Kwa upande wake Mwanahabari mkongwe nchini Tanzania, Fili Karashani, aliwataka watangazaji kuangalia maadili zaidi badala ya kujali fedha wanazopewa na baadhi ya watu ili kutengeneza vipindi au kurusha maneno yanayoweza kuleta mtafaruku kwenye jamii.

Huku akitoa mifano ya baadhi ya watangazaji wa Dar es salaam ambao wengi wao hupenda fedha ili kutangaza vipindi, alikemea tabia hiyo ambayo alisema ni sawa na kuuza utu wake kwa fedha kidogo ambazo haziwezi kukidhi mahitaji ya kila siku.

Karashani ambaye aliwasilisha mada iliyosema “Maadili ya Utangazaji kwenye Radio na Televisheni changamoto zake ni zipi”,aliwasihi watangazaji hao kuzingatia maadili ili kuiko jamii ya Tanzania ambayo sasa inaelekea kuacha maadili ya asili.

TCRA imekuwa ikitoa semina za mara kwa mara kwa watangazaji na wandaaji wa vipindi ambapo mwishoni mwa kila mwaka huwaita wote toka sehemu mbalimbali nchini ili kukumbushana na kuelekezana mambo mapya

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.