TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein amefanya uteuzi wa Manaibu Makamo Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar(SUZA).
Kwa mujibu wa taarifa iliotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi,Zanzibar Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee imeeleza kuwa Dkt Shein amemteuwa Dkt.Zakia Mohammed Abubakar kuwa Naibu Makamo Mkuu wa SUZA ataeshughulikia masuala ya Utawala.
Pia Dkt Shein amemteuwa Dkt Haji Mwevura kuwa Naibu Makamo Mkuu wa Chuo hicho atakaeshughulikia masuala ya Taaluma.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein amefanya uteuzi huo kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu10(1)cha Sheria ya SUZA namba 8 ya mwaka 1999 kama ilivyorekebishwa na kifungu cha 4 cha Sheria namba 11 ya mwaka 2009.
Uteuzi huo umeanza jana.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR
No comments:
Post a Comment