Habari za Punde

Dk Shein awataka viongozi wa serikali za mitaa kufanya kazi kwa pamoja

Na Rajab Mkasaba, Pemba
 
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapiduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein amewataka viongozi wa Serikali za Mitaa wakiwemo Madiwani na Masheha kisiwani Pemba kufanya kazi kwa pamoja kwani wana wajibu wa kuwatumikia wananchi na hakuna sababu ya kutohiltalifiana.

Kazi ya kuwatumikia wananchi imekuwa na changamoto nyingi hivyo ushirikiano na jitihada pamoja na kusaidiana kunahitajika kwani hilo ni la watu wote si la Masheha na Madiwani pekee.

Dk. Shein alisisitiza sana kufanya kazi kwa kushirikiana na kufanya kazi kwa pamoja na kutokafnya kazi kienyeji na wajue kuwa kila kitu kinakwenda kwa mujibu wa Katiba, Sheria na Kanuni ziliopo na haiwekani kufanywa nje ya hapo.

Alieleza imani yake baada ya maada alyoitoa Mkurugenzi wa vitambulisho hatarajii watu kuzozana na matarajio yake kuwa watu wote watafanya ipasavyo na kuwashajiisha watu kwenda kuchukua vitambulisho vyao kwani hilo sio suala la chama.


Alisema kuwa si jambo la kulishabikia isivyopaswa badala yake ni muhimu kujua nchi inaongozwa na Katiba na Sheria ilivyo, alisema kuwa tokea Mapinduzi kumekuwa kukifuatwa sheria na taratibu za nchi na si vyenginevyo.

Aliwaeleza kuwa iongozi hao ni lazima wajue kuwa wao ni watumishi wa wote na ni lazima wabadilike kwa kuwatumikiwa wananchi na wafuate sheria, Katiba na kutoa wito wa kuongeza kasi katika kufuata taratibu zilizowekwa pamoja na kufanya kazi kwa bidii.

Aliwaeleza kuwa siku za mbele semina kama hiyo itafanywa tena kwa lengo la kufikia yaliokusudiwa na kuhakikisha kuwa atahakikisha anayafuatilia maazimio yote yalitolewa katikas emina hiyo kwa kila wadi na Shehia.

Maelezo hayo aliyatoa katika ufungaji wa semina ya viongozi wa Serikali za Mitaa ambayo pia ilijikita katika suala ima la kuimarisha uhusiano baina ya viongozi wa kisiasa na kiutendaji iliyoanza tarehe 26 mwezi huu iliyofanyika huko katika ukumbi wa hoteli ya Misali, Wesha Pemba yenye kauli mbiu isemayo ‘viongozi lazima tubadilike’.

Katika maelezo yake, Dk Shein alisema kuwa viongozi hao wameonesha umakini wao katika siku zote tatu na kudhihirika kuwa kazi hiyo iliyofanywa ina manudaa kwani kuna haja ya kukaa pamoja ili kujenga mustakabali mzuri wa kuwatumikia wananchi wa Zanzibar.

Aliipongeze sekterieti iliyoongozwa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi kwa kufanikisha semina hiyo.


Akichangia mada ya ‘Wajibu wa Serikali za Mitaa katika kuimarisha utalii kwa wote’, Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad alisema kuwa vurugu zinazosababishwa na baadhi ya Jumuiya za kidini hapa Zazibar hazijengi utalii na badala yake vinabomoa mustakbali mzuri wa amani na utulivu iliyopo nchini.

Alisema kuwa kutokana na vurugu hizo zinazofanywa na Jumuiya hizo imezipelekea nchi mbali mbali zilizoendelea kuzihusisha Jumuiya hizo na vikundi viovu vinavyovuruga amani katika nchi kadhaa duniani.

Pamoja na hayo, Maalim Seif aliwataka viongozi hao wa Serikali za Mitaa kuhakikisha ulnzi na usalama kwa wageni unafanyiwa kazi kwani kumejitokeza tabia ya kuwapora watalii. Pia, alisisitiza kuimarishwa kwa utalii wa ndani.

Mapema akitoa mada kuhusu sekta hiyo, Mkurugenzi Mkuu, Kamishna ya Utalii Zanzibar Al Khalil Mirza alisisitiza kuwa msingi wa dhana ya ‘Utalii kwa Wote’ ni kuwashirikisha wananchi wa rika zote kushiriki kikamilifu katika uendelezaji wa sekta ya utalii hasa kwa wavuvi, wakulima, wajasiriamali na sekta nyengine za biashara ikiwemo hoteli na mikahawa.

Alisema kuwa utalii huo ni utalii ambao utakuwa na uwezo wa kupunguza au kuondosha madhara ya kiuchumi, kijamii, kiutamaduni na kimazingira.

Aidha dhana hii italeta faida kwa watu kwa akuweza kutumnza na kuendeleza mila na desturi zake.

Mkurugenzi Mkuu huyo alieleza kuwa imeonekana kuwa ipo haja ya kutoa fursa zaidi kwa jamii kushirikikatika kusimamia, kuendeleza na kuimarisha sekta hii kwa kushirikiana na vyombo simamizi vya Serikali.

Akieleza changamoto zilizopo Mkurugenzi Mirza alieleza kuwa kukosekana kwa amani kunaathiri sana sekta ya utalii kwani kutokuwepo kwa amani na utulivu hupelekea wageni walio wengi kutotembelea katika eneo hilo.

Mgongano wa miono baina ya wenyeji na watalii, uharibifu wa mazingira pamoja na kuacha vijana kuiga mambo ya kigeni bila ya kuzuizi husababisha mporomoko wa maadili.

Akitoa mada iliyohusu Wajibu wa Masheha katika uandikishaji wa Mzanzibari Mkaazi, Mkurugezi, Ofisi ya Usajili na Kadi za Utambulisho, Mohammed Juma Ame alisema kuwa ili kufanikisha usajili wa Wazanzibari Sheha ana wajibu wa kutibitisha kuwa anayeomba kusajiliwa anazo sifa za Mzanzibari Mkaazi.

Mkurugenzi huyo pia, alieleza kuwepo kwa udanganyifu mkubwa wa vyeti vya kuzaliwa hivi sasa huku akieleza kuwa Idara yake haitolifumbia macho suala hilo na badala yake sheria itachukua mkondo wake.

Katibu wa Baraza la Mapinduzi alisema kuwa maazio yote yaliopatikana Unguja na Pemba yatawekwa pamoja na baadae kuhakikisha kila kiongozi wa Serikali za mitaa anapata maazimio hayo.

Mapema Dk. Abdulhamid alieleza kuwa kila mtu awe na dhima ya kufuata desturi na mila ziliopo na isitolewe kisingizio scha kuja kwa watalii na kueleza kuwa suala la kuimarisha maadili na kutofuata silka nyengie ni uamuzi wa wananchi wenyewe kuamua wageni wanaokuja wavae vip na wawe vipi

Viongozi hao pia walisisitizwa umuhimu wa kuimarisha Utawala Bora, mada iliyotolewa na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.