Kulia yake ni Muanzilishi wa Mradi wa Taa hizo wa Kampuni ya Wakawaka Bwana Maurits Groenna kushoto yake ni Mkurugenzi Masoko wa Kampuni hiyo Bwana Bill Carey
Muanzilishi wa Mradi wa Taa zinazotumia mwanga wa Jua wa Kampuni ya Wakawaka ya Nchini Uholanzi Bwana Maurits Groen akifahamisha namna ya matumizi sahihi ya Taa zinazotumia mwanga wa jua kwa Wananchi wa Kijiji cha Matetema na Kichungwani ndani ya Jimbo la Kitope ambao walibahatika kupata msaada huo.
Kushoto yake ni Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi na Kulia ni Mkurugenzi masoko wa Kampuni ya Wakawaka Bwan Bill Carney.
Mbunge wa Jimbo la KitopeBalozi Seif Ali Iddi akimkabidhi mmoja miongoni mwa wananchi kadhaa wa Vijiji vya Matetema na Kichungwani Taa inayotumia mwanga wa jua zilizotolewa msaada na Kampuni ya wakawaka ya nchiniUholanzi.
Muanzilishi wa Mradi wa Taazinazotumia mwanga wa Jua kutoka Kampuni ya Wakawaka ya Nchini Uholanzi Bwanan Maurits Groen akimkabidhi Taa inayotumia mwanga wa jua mmoja wa wananchi kadhaa wa Vijiji vya Matetema na Kichungwani ndani ya Jimbo la Kitope.
Na Othman Khamis Ame
Kampuni inayojishughulisha na mradi wa Umeme unaotumia Jua {Solar Energy } yenye Makao Makuu yake Nchini Uholanzi ya Wakawaka imetoa msaada wa Taa Mia Nne zinazotumia nguvu za mwanga wa jua kwa Vijiji viwili vya Matetema na Kichungwani vilivyomo ndani ya Jimbo la Kitope Wilaya ya Kaskazini B.
Halfa ya ugawaji waTaa hizo imesimamiwa na Mbunge wa Jimbo hilo Balozi Seif Ali Iddi pamoja na Mkurugenzi Masoko wa Kampuni ya Wakawaka Bwana Bill Carney ambapo jumla ya Nyumba 86 za Kijiji cha Matetema na160 za Kijiji cha Kichungwani zilipata mgao wa Taa moja kwa kila nyumba.
Jumla ya shilingi Milioni 25,000,000/- zimetumika kutengenezea Taa hizo mia Nne zitakazosaidia kupunguza matumizi makubwa ya Taa za Vibatari zinazotumia Mafuta ambapo kila taa moja ina Thamani ya Shilingi Sitini elfu {60,000/- }.
Akizungumzana Wananchi wa Vijiji hivyo vya Matetema na Kichungwani kwa nyakati tofauti Muanzilishi wa Mradi huo waTaa zinazotumia mwanga wa Jua kutoka Kampuni ya Wakawaka Bwana Maurits Groenalisema Kampuni yao imeamua kuanzisha mradi huo kwa lengo la kusaidia Jamii yenye kipato cha Chini katika Mataifa mbali mbali Duniani.
Bwana Maurits alisema Jamii kubwa hasa katika Mataifa maskini zimekuwa zikitumia gharama kubwa kwa ununuzi wa mafuta kwa ajili ya matumizi ya Taa jambo ambalo linawaongezea mgizo wa matumizi wakati kipato chao ni hafifu.
Alisema pia yapo matatizo yauchafuzi wa mazingira pamoja na ajali za mara kwa mara za moto zinazosababishwa na matumizi makubwa ya Taa za Vibatari ambazo huleta athari na wakati mwengine maafa kutuokana na Taa hizo.
Naye Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi aliipongeza Mampuni hiyo ya Wakawaka ya Nchini Uholanzi kwa uamuzi wake wa kusaidia Wananchi wa Jimbo la Kitope katika kujipatia huduma za Taa zinazotumia mwanga wa Jua.
Balozi Seifambaye pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema Taa hizo kwa kiasi kikubwa zitaweza kusaidia matumizi mbali mbali majumbani likiwemo lile muhimu la wanafunzi kupata wasaa wa kudurumu masomo yao.
Alisema kwaVile Tanzania na Zanzibar kwa ujumla zimebahatika kuwa na kipindi kirefu cha Juandani ya mzunguko wa mwaka wa miongo yake Taa hizo zitakuwa na uwezo wa kutoa huduma kwa kadri ya lengo lililokusudiwa la kuanzishwa kwa mradi huo.
“ Haya ni maendeleo ya kuachana na Taa za Vibatari kwa vile tayari tumeshakuwa na Taa isiyohitaji mafuta ambayo ni gharama na yanachafua mazingira”. Alisema Balozi Seif.
Mradi huo wa Kampuni ya Wakawaka wa Taa zinazotumia mwanga wa Jua ni wa mwanzo kuingia ndani ya Bara la Afrika ukiwa ni wa majaribio.
Mbunge huyo wa Jimbo la Kitope akiambatana na Ujumbe wa Uongozi wa Kampuni hiyo ya Wakawaka inayosimamia mradi wa Taa zinazotumia mwanga wa Jua walipata fursa ya Kuangaliwa Umeme unaotumia jua kwa baadhi ya Nyumba na Msikiti uliopo katika Kijiji hicho cha Kichungwani.
Muanzilishi wa Mradi wa Taa hizo Bwana Maurits Groen alimueleza Balozi Seif kwamba Kampuni yake ina uwezo wa kila hali kutengeneza Vifaa vya Umeme unaotumia mwanga wa jua.
Angalia viongozi wetu walivyokuwa hawana akili ikisha huyu ndio kasahawahi kuwa mpaka balozi, na sasa hivi ndio Makamo wa Raisi, manaake si mtu ambae hajui siasa za duniani zinavyokwenda, sifikirii kama mambo kama haya yanatakiwa yawe kisiasa kwasababu yeye si kiongozi wa wanachama wa CCM tu kuna sehemu anatakiwa aonyeshe tofauti baina ya kuwa yupo kichama au kiongozi wa serikali kwa hali hii hatufiki abadan...."NYINYI VIONGOZI WAJINGA BADILIKENI JAMANI WACHENI AKILI MBOVU"..... AAAAAAAHHHHHHHHHHH INAUDHI HASWA MAMBO MENGINE HASWA KUONA
ReplyDelete