Habari za Punde

Mamlaka ya viwanja vya ndege watakiwa kuacha kufanya kazi kwa mazoea

Na Nafisa Madai WMM

 Wafanyakazi wa mamlaka ya viwanja vya ndege Zanzibar waache kufanya kazi kwa mazoea na badala yake wakubali kubadilika na kuhakikisha kila mmoja anapokwenda kazini afuate majukumu yake ya kazi aliyopangiwa. 

 Hayo yameelezwa jana na waziri wa miundombinu na mawasiliano mhe Rashid Seif Suleiman alipokua akizungumza na wafanyakazi hao katika kikao chake cha kwanza tokea ateuliwa kuongoza wizara hiyo baada ya kufanya ziara katika taasisi mbali mbali za mamlaka hiyo. 

 Aidha alisema kuwa utendaji wa kazi lazima uwe na malengo na sio kusukumana kwa kila mtu aweze kujitathmini tokea anapofika kazini amewajibika ipasavyo. 


 Hata hivyo amesema wizara ya miundombinu ni wizara ambayo inayoyotoa huduma moja kwa moja hivyo aliwataka wafanyakazi hao kuwa lugha nzuri wanapotoa hudma zao kwa wateja ili waweze kujitangaza zaidi.

 Kwa upande wao wafanyakazi hao kutoka vitengo tofauti wamesema sehemu zao za kazi zinakabiliwa na changamoto kubwa ya vitendea kazi na kukosa elimu ya ziada ambayo itaweza kusaidia utendaji wao. 

 Mbali na changamoto hizo wafanyakazi hao wameomba wapatie mashirikiano makubwa kutoka kwa viongozi wakuu wa serikali kwani wao ndio watumiaji wakuu wa kiwanja hicho 

 Katika ziara hiyo mhe Rashid alipata fursa ya kutembelea kitengo cha zimamoto ambako aliweza kupata maelezo kutoka kwa mkuu wa kitengo hicho ambae alisema katika kitendo hicho wanakabiliwa na changa moto kubwa ya elimu ya ziada ambayo yatawezesha kitengo hicho kuwa cha kisasa. 

 Aidha waziri huyo alitembelea VIP mpya,ujenzi wa Departure na Parking za magari ambapo mkuu wa kitengo hicho ndugu Yassir dicosta alitoa maelezo mafupi ambaapo alisema hivi sasa kuna mabadiliko ya mtiririko wa abiria baada ya kuhamisha mashine nje. 

 Sehemu nyengine alizotembelea ni pamoja na depacha ndani na first class lounge,choo cha madawa ya kulevya, jengo jipya la abiria,eneo la uzio pamoja na kutembelea eneo la uzio kwa ndani kupitia SOGEA SATOM ofisi,hadi substation B Jeshi, eneo la mitambo na mwisho kutembelea eneo linalotarajiwa kujengwa TAXIWAY.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.