Habari za Punde

Mwenyekiti wa AFP asisitiza vijana wapewe ajira

Na Mwanaisha Mohammed, Maelezo
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohammed Shein amekumbushwa kuyafanyia kazi mazungumzo juu ya kuwapatia vijana wa Zanzibar ajira ili waondokane na hali ngumu ya kimaisha.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara Ya Habari Maelezo Rahaleo Mwenyekiti wa Chama Cha Wakulima Tanzania (AFP)Said Soud Said alisema kuwa endapo vijana wakipatiwa ajira itakua ni njia ya kuondokana na matatizo yanayowakabili katika harakati za kuendesha maisha yao.
Alisemakuwa kwa upande wao Chama Chao kilimshauri Rais kujenga viwanda vitatu vya minofu ya samaki hapa Zanzibar ambapo vijana wengi wataweza kuajiriwa katika viwanda hivyo

Soud alisema kuwa mbali na suala hilo ,pia vijana wangeliweza kupatiwa msaada wa kulima mashamba ya mboga ambayo yataweza kusaidia kuwapatia kipato chao na kuondokana na bidhaa hiyo kuagiza kutoka nje.
Mwenyekiti huyo alisikitishwa na hali iliopo hivi sasa kutokana na fedha nyingi za wananchi wa Zanzibar kutumika nje ya Zanzibar kwa kununua mboga mboga wakati fedha hizo zingefaa kwa kujiletea maendeleo.
Akizungumzia juu ya hali ya amani ya nchi alisema kuwa hivi sasa vimejitokeza baadha ya vikundi vya dini ambavyo vinaonekana vikikiuka taratibu za nchi ambazo vinasababisha uvunjifu wa amani.
Mwenyekiti huyo wa chama cha AFP alisema kuwa baadhi ya vyama hivyo vimejisajili kuhubiri dini lakini badala yake kufanya vitendo vya kuhatarisha amani ya nchi jambo ambalo ni kinyume na sheria walizosajiliwa.
Hata Hivyo alisema kuwa wanajamii wawe wanaitikia wito wa kutoa maoni juu ya mchakato wa katiba ili kuondokana na migogoro ya Muungano na nchi kuwa katika hali ya amani na utulivu.
Vile vile Mwenyekiti huyo alisema kuwa Zanzibar ilikuwa ni nchi yenye utulivu ila kutokana na makundi ya watu yanayojotokeza kumekua na vurugu za mara kwa mara hivyo ni jukumu la viongozi kuhakikisha kuwa kunawekwa ulinzi wa hali ya juu.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.