Habari za Punde

Mabadiliko ya kuanza Muhula mpya wa masomo Suza 2012/2013



PRESS RELEASE

THE STATE UNIVERSITY                                     CHUO KIKUU CHA TAIFA

OF ZANZIBAR                                                         CHA ZANZIBAR

P. O. Box 146                                                            S. L. P. 146

Tel: 255-24-2230724/2233337                              Simu: 255-24-2230724/2233337

ZanzibarTanzania                                               Zanzibar - Tanzania

Fax: 255-24-2233337                                              Fax: 255-24-2233337

E-mail:vc@suza.ac.tz                                             E-mail: vc@suza@ac.tz

 

Septemba 26, 2012

 

MABADILIKO YA KUANZA KWA MUHULA MPYA WA MASOMO 2012/2013.

Uongozi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA), unawaarifu wanafunzi, wazazi na walezi wa wanafunzi kuwa, kutokana na sababu zisizoepukika, umesogeza mbele tarehe ya kuanza mwaka mpya wa masomo wa 2012/2013 kama ifuatavyo:-
Kwa wanafunzi wapya watafungua tarehe 29 Oktoba, 2012 kwa ajili ya wiki ya matayarisho (orientation week) na wanafunzi wanaoendelea masomo yataanza tarehe 05 Novemba, 2012.
Wanafunzi wote wanatakiwa walipe asilimia hamsini (50%) ya ada ya masomo yao ndani ya wiki ya mbili za mwanzo na ndipo watafanyiwa usajili.
Kwa utaratibu zaidi wa kujua wanafunzi watakaosomea Kampasi Tunguu na Nkrumah watembelee  tovuti ya  Chuo  www.suza.ac.tz

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.