Habari za Punde

Rais wa Zanzibar Dk. Shein Azinduwa Mfuko wa Walemavu Zanzibar. Zanzibar Beach Mazizini.N


 
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akizinduwa Mfuko wa Watu Wenye Ulemavu Zanzibar katika Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Mazizini.
 Waalikwa wakimsikiliza Rais wa Zanzibar Dk. Shein akiwahutubia katika sherehe za Uzinduzi wa Mfuko wa Watu wenye Ulemavu Zanzibar.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad, akitowa mchango wake wa Shilingi Milioni Sita kwa kuchangia Mfuko wa Watu wenye Ulemavu Zanzibar, wakati wa uzinduzi wake katika hoteli ya Zanzibar Beach Mazizini.
  Waheshimiwa wakisikiliza hutuba ya Uzinduzi wa Mfuko wa Watu wenye Ulemavu Zanzibar.
Mwenyekiti wa Mfuko wa Watu wenye Ulemavu Zanzibar na Waziri wa Biashara Viwanda Masoko Nassor Mazrui akitowa maelezo ya Mfuko huo wakati wa uzinduzi wake uliofanywa na Rais wa Zanzibar, katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Mazizini Zanzibar.
Wageni waalikwa wakifuatilia Uzinduzi wa Mfuko wa Walemavu Zanzibar.
  Mchoraji wa Picha ya Rais wa Zanzibar,Dk. Ali Mohamed Shein, Mahmoud Hemeid, akiwa na picha hiyo wakati ikipingwa Mnada kwa ajili ya Fedha hizo kuchangia Mfuko wa Walemavu katika Uzinduzi wake hoteli ya Zanzibar Beach Mazizini.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimkabidhi mnunuzi wa picha hiyoi ya kuchora Mrs. Fortunata Temu,wa Kampuni ya SWISSPORT. baada ya kuinunua klwa shilingi milioni 1.5, katika mnada ulionadishwa katika ukumbi huo wakati wa Chakula cha Usiku kilichoandaliwa kwa Uzinfuzi wa Mfuko huo.
Mchoraji wa Picha ya Rais wa Kwanza wa Zanzibar,Marehemu Mzee Abeid Amani Karume, Mahmoud Hemeid, akiwa na picha hiyo wakati ikipingwa Mnada kwa ajili ya Fedha hizo kuchangia Mfuko wa Walemavu katika Uzinduzi wake hoteli ya Zanzibar Beach Mazizini.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Zahra Hamad, akikabidhiwa picha ya Mzee Karume baada ya kuinunua katika Mnada kwa Shilingi Milioni 1.2. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akizindua Tovoti ya Mfuko wa Watu wenye Ulemavu Zanzibar, wakishangilia Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdallah Mwinyi Khamis na   Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Fatma Ferej.
Viongozi wa Meza kuu wakifuatilia Ngoma ikichezwa na Watu wenye Ulemavu wa kutosikia, wakati wa Uzinduzi waxMfuko wa Watu wenye Ulemavu Zanzibar.
Wasanii wa Kikundi cha Walemavu wa Kutokusikia wakitowa burudani ya ngoma katika sherehe za uzinduzi wa mfuko wa Walemavu Zanzibar.
Waalikiwa wakishangilia kwa ishara kuashirika kupiga makofi kwa kuinua mikono juu.
Rais wa Zanzibar akisalimiana na Wasanii wa Kikundi cha Watu wenye Ulemavu wa kutokusikia baada ya kutoa burudani ya ngoma.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar wakujumuika katika Chakula Maalum kilichoandaliwa kwa ajili ya kuchangia Mfuko wa Walemavu Zanzibar. 
Wasanii wa Kikundi cha Watu wanye Ulemavu wa kutokusikia wakipata chakula cha usiku kilichoandaliwa kwa ajili yao kuchangia mfuko wa Walemavu Zanzibar.
Walemavu wa kutokuona wakisoma utenzi maalum katika sherehe za kuchangia Mfuko wa Walemavu Zanzibar, kulia Awena Hassan Mwanafunzi wa kidatu cha kwanza Mchipuo Skuli ya Vikokotoni na Jamila Borafia mwanafunzi wa skuli ya msingi Kisiwandui.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akikabidhiwa mfano wa Cheki ya Shilingi Milioni 15, 000,000/= na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano wa Kampuni ya simu ya VODACOM Tanzania, Joseline Kamuhanda.na Salum Mwalimu Meneja Mahusiano ya Nje.  
Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF,Abdulwakili Hafidhi, akimkabidhi mfano wa cheki ya Shilingi Miliono Kumi kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, ikiwa ni mchango wao kwa Mfuko wa Watu wenye Ulemavu Zanzibar. anayeshuhudia Afisa Uhusiano wa ZSSF Mussa Yussuf.
Afisa Uhusiano Muandamizi wa Mfuko NSSF Tanzania, Theopista ,J.Muheta akimkabidhi cheki ya Shilingi Milioni Kumi. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, ikiwa ni mchango wa Mfuko wa Watu wenye Ulemavu Zanzibar wakati wa sherehe za Uzinduzi wa Mfuko huo.
Mfanyabiasha maarufu Tanzania Yussuf Manji akiponghezwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, kwa mchango wake kwa kuchangia Mfuko wa Watu wenye Ulemavu Zanzibar wakati wa sherehe hizo zilizofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Beach Mazizini.
Mkurugenzi wa Benki ya Watu wa Zanzibar PBZ, Juma  Amour, akipongezwa na Rais wa Zanzibar kwa benki yao kuchangia Mfuko wa Watu wenye Ulemavu Zanzibar.
Mfanyabiashara wa Zanzibar Suleiman Hawaii, akimkabidhi mchango wake wa shilingi Milioni Tano kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi katika Uzinduzi wa Mfuko wa Watu wenye Ulemavu Zanzibar.
Mfanyabiashara wa Zanzibar Jeff Babu, akimkabidhi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein. mchango wake wa Dola 500/= kwa ajiuli ya mfuko wa Walemavu Zanzibar.


Mkalimani wa lugha kwa ishara kwa wanye ulemavu wa kutokusikia katika sherehe za uzinduzi wa mfuko wa watu wenye ulemavu zanzibar. 


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.