BaloziMpya wa India Nchini Tanzania Bwana Debnath Shaw akizungumza na Makamu wa Piliwa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddialiyefika Zanzibarkujitambulisha Rasmi
Makamu waPili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimshukuru Balozi Mpya wa IndiaNchini Tanzania Bwana Debnath Shaw baada ya kupokea zawadi na kumalizamazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar
Na Othman Khamis Ame
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaangalia mazingira ya kuimarisha pamoja na kuvifufua Viwanda Vidogovidogo ili kuongeza soko la ajira sambamba na kupata mbinu za usindikaji wamazao mbali mbali yanayozalishwa hapa Nchini.
Makamu wa Pili wa Rais wa ZanzibarBalozi Seif Ali Iddi alieleza hayo wakati akizungumza na Balozi Mpya wa India Nchini Tanzania Bwana Debnath Shawaliyefika Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar kujitambulisha rasmi.
Balozi Seif alisema Zanzibarimekuwa na historia kubwa ya masuala ya Viwanda vidogo vidogo hasa katika miakaya thamanini jambo ambalo lilileta faraja kwa bidhaa za Zanzibar katika Soko la Mataifa ya Mwambao waAfrika Mashariki.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibaralimuomba Balozi huyo wa IndiaNchini Tanzania kuyashawishiMakampuni ya Nchi yake kuitumia fursa hiyo ya uwekezaji katika sekta ya Viwandakwa lengo la kusaidia Uchumi wa Zanzibarsambamba na kuongeza mapato ya Makampuni hayo.
Balozi Seif aliipongeza na kuishukuru Serikali yaIndia kwa hatua yake inayochukuwa ya kuunga mkono harakati za Maendeleo zaZanzibar hasa katika masuala ya Uhandisi, Afya na Elimu.
Alisema idadi ya Wanafunzi wa Zanzibarwanaopatiwa mafunzo mafupi na marefu Nchini India imeongezeka zaidi na kuletaufanisi katika Taasisi za Serikali.
“ Ongezeko la idadi ya Wanafunzi wa Zanzibarwanaopata Taaluma Indiaimesaidia kuimarisha uhusiano zaidi waKiuchumi na Ustawi wa Jamii kati yetu na Nchi hiyo”. Alifafanua Balozi Seif.
Alimuhakikisha Balozi huyo mpya wa India Nchini Nchini Tanzania kwamba Uhusiano huo wamuda mrefu kati ya pande hizo mbili utazidi kudumishwa kwa faida ya jamii yaWananchi wa Nchi hizo.
Mapema Balozi Mpya wa IndiaNchini TanzaniaBwana Debnath Shaw alisema katika kuungamkono Mataifa ya Bara la Afrika Nchi yake yake tayari imeshaandaa Mpango wakuongeza ushirikiano wake na Mataifahayo ndani ya kipindi cha Miaka mitano iliyopita.
Balozi Debnath alisema mpango huo umelenga zaidi kuyaongezeanguvu za kiuchumi Mataifa hayo katika masuala ya Taaluma na uwekezaji kwenyeSekta ya Afya.
Wakati huo huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif AliIddi alikutana na Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano waKimataifa Zanzibar Balozi Silima K. Haji aliyefika kujitambulisha baada yakuteuliwa kushika wadhifa huo hivi karibuni.
Katika mazungumzo yaoyaliyofanyika Ofisini kwake Vuga Mjini ZanzibarBalozi Seif alisema Idara hiyo ni muhimu kwa vile imeundwa maalum kwa ajili ya itifaki ya Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibaralimueleza Balozi Khamis kwamba Zanzibarhivi sasa iko katika muelekeo mpya wauendeshaji wa Serikali katika mfumo wa Umoja wa Kitaifa.
Hivyo aliiomba Taasisi hiyo muhimu kutumia nguvu zakekatika kuhakikisha inaitangaza Zanzibar kimataifa ili ieleweke kutokana na mfumo huompya.
Alisema yapo matumaini makubwa ya Serikali yaMapinduzi ya Zanzibarkuendelea kuwa imara kutokana na uwakilishi wa Viongozi wa pande zote mbiliambazo zilikaribiana katika matokeo ya kura katika uchaguzi Mkuu uliopita.
No comments:
Post a Comment