Habari za Punde

Uharibifu wa Mazingira katika Makaburi ya Wakristo Mwanakwerekwe

 Katibu wa Kanisa la Anglikan Mkunazini Zanzibar Nuhu Salanya, akionesha eneo la ukuta uliojengwa na Kanisa ili kuhifadhi eneo hilo ukiwa umevunjwa na kuchukulewa sehemu kubwa ya eneo hilo kwa makazi na uchimbaji wa mchanga, wakati walipofanya ziara na waandishi wa habari na Viongozi wa Wilaya ya Magharibi kujionea uharibifu huo wa mazingira katika eneo hilo kwa kuwa na mashimo katika maeneo ya makaburi.  
 Viongozi wa Umoja wa Makanisa Zanzibar na Waandishi wa habari na viongozi wa Halmashauri ya Wilaya wakitembelea eneo hilo kujionea wenyewe uharibifu wa mazingira unavyofanyika katika eneo hilo na Wananchi wasiopenda kutunza mazingira ya maeneo yao.  
 Askofu wa Kanisa la Assemble of God Zanzibar Dicson Kanganasi akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uharibifu huu unaofanywa na Wananchi katika maeneo ya kuzikia ambayo hutumiwa na Waumini wa dini ya Kikristo Zanzibar yakiwa na yamekuwa katika hali ya kuaribika kimazingira kwa kuwa na mashimo kwa ajili ya kuchimba mchanga na kuhatarisha makaburi kuwa wazi kutokana na uchimbaji huo.
 Viongozi wa Umoja wa Makanisa Zanzibar wakiangalia moja ya kaburi likiwa katika hali ya uharibifu wa mazingira kwa kuchimbwa mchanga na kuhatarisha mifupa ya binaadamu aliyezikwa hapo kuwa nje baada ya muda mfupi ikinyesha mvua na mchanga wake kuporomoka.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.