Habari za Punde

Zoezi la Uchaguzi Mdogo Jimbo la Bububu Ulivyokuwa

Wananchi wa Jimbo laBububu wakiangalia majina yao katika kituo cha wapiga kura katika Skuli yaMsingi Bububu kujua chumbakipi wanapiga kura yao katika zoezi la uichaguzi mdogo wa jimbo la bububu.
Wananchi wa jimbo la bububu wakiwa katika mstari kusubiri kupiga kurakatika kituo cha skuli ya msingi bububu.
Ofisa wa kituo cha kupigia kura katika skuli ya msingi bububu akiwa na kura ya inayodaiwa nampiga kura kuwa imeharibika ikiwa na mchoro nje.
Mwananchi akimsaidia Mwananchi Fatma Ali  mwenye ulemavu kuvuka barabara baada ya kupiga kura yake ikiwa ni moja ya haki yake ya msingi kumchagua  Mgombea amtakae. katika uchaguzi mdogo wa jimbo la bububu
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi aliyeinua mkono akiwa na wasaidi wake akitowa maelekezo kuhakikisha amani na utulivu inaendelea kuwepo katika zoezi la upigaji kura katika kituo cha bububu.
Mkaazi wa Bububu Mshelishelini Mohammed Bushir, akisaidiwa na mwanawe kuigia katika kituo cha kupigia kura katika Chuo cha Taifa SUZA 
Mwananchi wa Shehia ya Kibweni akipiga kura yake katika kituo cha Batras.
Mawakala wa Vyama vya Siasa wakiangalia jina la mpiga kura aliyefika katika kituo cha kupigia kura kama yuko katika daftari la wapiga kura wa jimbo la bububu. wakati wa uchaguzi mdogo wa jimbo hilo.
Maofisa wa Upigaji kurawa Kituo cha Chuo cha Taifa  SUZA, wakihesabu kura  baada ya kumaliza kupigisha kuwa Wananchi wa Jimbo la Bububu katika uchaguzi mdogo wa jimbo hilo uliofanyika jumapili. 
Mawakala wa Vyama vya Siasa vilivyoshiriki Uchaguzi Mdogo waJimbo la Bububu wakisimamia uhesabuji wa kura katika kimoja ya kituo cha kupigia kura.  
Mgombea Uwakilishi kupitia Chama cha CUF Issa Khamis Issa, kushoto akiwa na Wakala wa  Chama chake Mbunge wa Magogoni Hamad Ali Hamad, wakijadili kituo wakiwa kituo chakupigiakura cha Betras baada ya kumaliza zoezi la kupiga kura katika kituo hicho.
Mgombea Uwakilishi waChama cha CUF, Issa Khamis Issa akiwa na Msimamizi waUchaguzi wa Chama cha Mapinduzi MzeeTakrima wakiwa nje ya  kituo cha skuli ya bububu.
Ofisa wa kituo cha kupigia kura akimueka wino  maalum mmoja wa wapiga kura kuonesha kuwatayari ameshapika kura yake katika kituo cha skuli ya bububu.
Wagombea Uwakilishi katika Uchaguzi Mdogo waJimbo la Bububu, Issa Khamis Issa (CUF) na Hussein Ibrahim Makungu (CCM)  wakiwa katika viwanjavya kupigiakurakatikaSkuli yaBububu wakifuatilia zoezi laUchaguzi linavyokwenda na nani ataibuka mshinda katikazoaezi hilo, wakiteta na kutambiana.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.