Habari za Punde

ANC iko Zanzibar kujifunza namna ya kuendesha Baraza la Wawakilishi

 
Na Ali Issa Maelezo Zanzibar

Mnadhimu Mkuu wa chama Tawala (ANC)katika Bunge la Afrika Kusini Phel Parkies amesema kuwa ni vyema nchi za kiafrika kujenga umoja na kuenzi utamaduni wao katika kuendesha mabunge ya Nchi zao nakuacha desturi za Nchi za Magharibi .

Hayo ameyasema leo huko Vuga Mjini Zanzibar wakati ujumbe wa watu watano ulipokutana na Waziri wa nchi Afisi ya Makamu Wapili wa Rais Mohamed Aboud Mohamed waliofika Ofisini hapo kujifunza namna ya uendeshaji wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.

Amesema ni vyema kwa nchi hizo kuacha utamaduni wa kigeni kwani Bara la Afrika limesheheni utamaduni uliobora na unakubalika na kuthaminiwa na mataifa yote duniani kutokana na mila zao.

“Namna tunavyoendesha vikao katika mabunge yetu pamoja na mavazi tunayovaa na uendeshaji wa serikali zetu bado unafuata mfumo wa nchi za magharibi na wakati umefika kuachana na utamaduni wao” alisema Phel Parkies .


Nae waziri Muhamed Aboud alisema kua ni kweli jambo hilo linawezekana kabisa lakini kitu cha msingi kwa Nnchi za Afrika kujithamini na kuona utamaduni wao ni bora kuliko utamaduni wa magharibi unaendelea kuathiri nchi zao .
Aidha alisema kuwa hakuna lisilo wezekana kwani nchi ya China imepiga hatua kubwa ya maendeleo kutokana na kuthamini na kufuata utamaduni wa nchi yao bila ya kuingiza mila na silka za kigeni
Pia alisema kua kwavile Afrika ya kusini ni nchi kubwa na iliyopiga hatua kubwa za kimaendeleo ukilinganisha na nchi nyengine za Afrika, ni vyema kua mstari wa mbele katika kuonyesha njia mataifa mengine ya kiafrika kujinasua na athari za kimagharibi.
Waziri Abuod alisema katika kufikia lengo hilo ni vyema lugha ya Kiswahili ikapewa kipaumbele katika shughuli mbali mbali za kitaifa na kimataifa kwa vile kwa kiasi kikubwa inaonekana kua ni lugha ya Afrika nzima.

1 comment:

  1. Hapa naona kama wamekuja kutembea tu kwa sababu kama wanasema bunge lao huko Afrika kusini linafata mfumo wa kimagharibi hadi kwenye mavazi, sasa kwa Zanzibar sijui watajifunza nini kwani kila nikiangalia hilo baraza la wawakilishi sioni kama mavazi yanayovaliwa humo ni ya kizanzibari ama kiislamu au vp kwani watu wakiingia humo huwa wametinga vazi la suti au suti sio vazi la kimagharibi?, unaweza ukaona baadhi ya wajumbe wa baraza hilo wamevaa kanzu siku ya ijumaa tu, na pia hata huo mfumo wa uendeshaji hilo baraza lenyewe ni wa kimagharibi sasa hapa sijui watajifunza nini.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.