WACHEZAJI wa klabu ya Cossovo ya
Chumbageni, wakiwa katika furaha nono baada ya kujipitia goli la pili na
ushindi, lililofungwa na Juma Mchunga Bakar, kwenye mchezo wa fungua dimba wa
ligi daraja la pili Wilaya ya Mkoani, uliochezwa uwanja wa Aston Villa Wambaa
ambapo katika mchezo huo, timu ya Cossovo iliwabugiza watani wao hao timu ya
Maendeleo nayo ya Chumbageni kwa magoli 2-1 (picha na Haji Nassor, Pemba)
Na
Haji Nassor, Pemba
HATIMAE
ule ubishi uliokuwa umetawala, takriban wiki tatu zilizopita kwa timu za
Cossovo na Maendeleo zinazoishi mtaa mmoja wa Chumbageni ambazo zinashiriki
ligi daraja la pili Wilaya ya Mkoani, umemalizika jana baada ya timu ya Cossovo kuwakoromea watani wao hao kwa 2-1.
Katika mchezo huo wa fungua dimba uliopigwa
uwanja wa Aston Villa Wambaa na kuhudhuriwa na mamia ya wapenda soka wakiwa
pamoja na wanawake, ulinaza kwa kasi huku kila mmoja akitafuta njia ili aondoke
na ushidi uwanja hapo.
Cossovo ambapo kwa mara ya mwisho
walipokutana na Maendeleo ililala kwa idadai kama hiyo ya magoli, jana hiyo
iliakuwa ya mwanzo kuzichana nyavu za Maendeleo kwa kujipatia goli safi
lililowekwa kimiani na Juma Mchunga Bakar dakika ya 20, baada kuunganishiwa
jaro safi toka masharki mwa uwanja huo.
Kuingia kwa goli hilo Maendeleo walikuja juu, na kuhamia
mfululizi langoni mwa Cososovo kwa nia kusawazisha, lakini walijikuta
wakipunguzwa nguvu baada ya Juma Mchunga tena, dakika ya 30 kuiandikia timu
yake goli la pili lililodumu hadi mapunziko.
Kipindi cha pili kilianza kwa mkosi kwa
timu ya Cossovo, baada ya mshambuliaji wao hatari Mohamed Bakar (Ngasa), kulima
kadi nyekundu na mwamuzi wa mchezo huo Mwalimu Hussien ambapo hilo liliwapa faraja Maendeleo.
Dakika 49 baada ya kufanya mabadiliko ya
kumtoa Abdull-karim Omar na kumuingiza mkongwe Suleiman Ali, kuliamsha ari kwa
wachezaji hao, hali ambayo ilisababisha kujipatia goli la kufutia machozi,
lililowekwa kimiani kwa ufundi na Mohamed Abrhaman baada kuachia fataki zito.
Kuingia kwa goli hilo, timu ya Maendeleo ilionekana kupata
uhai na kusakata kambumbu vyema, lakini dakika 90 zikamalizika kwa Cossovo
kutoroka na alama tatau muhimu, ambapo pia katika mchezo mwengine uliopigwa
uwanja wa Mpikatanga timu ya Aston villa iliangukia pua kwa kuchupwa magoli 2-1
na News scard kutoka Mtambile.
Timu ya Cossovo itatupa katarata yeke tena
Oktoba, 21 kwa kuumana na Aston Villa, kwenye uwanja wa Wambaa, huku kaka zao
timu ya Maendeleo wakijaribu bahati yao
tena siku hiyo hiyo uwanja wa Makombeni kwa kutibuana na Jiondeni .
No comments:
Post a Comment