Wa pili kulia ni mkuu wa msafara ndugu Abdalla Kombo, afisa tawala wa wilaya ya kusini, akifuatiwa na ndugu Muombwa, msaidizi wa makamo wa pili wa Rais, Bi Zawadi Hamdu Vuai, Diwani wa wadi ya Mzuri Kaja, na ndugu Hassan, diwani wa wadi ya Kajengwa wakipata maelezo kuhusu Chuo cha Madini Kiruna, Sweden kutoka kwa Bi Anna, msaidizi wa Chuo hicho. Picha nyengine zinaonyesha chuo na sehemu mbali mbali. Chuo hiki kimekusanya madini kutoka nchi mbali mbali ikiwemo Tanzani ambapo madini ya Tanzanite pia yapo hapa kwenye makabati. Wanafunzi husoma chuo hiki kwa kipindi kirefu kuanzia miaka 3 hadi mitano na ukitoka chuo hiki unakuwa na uwezo wa kusarifu madini kimataifa.
Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza akisarifu madini ya fedha katika chuo cha Madini Kiruna. Kwa mujibu wa maelezo ya mwalimu kazi hii inahitaji utulivu wa akili. Ujumbe wa Makunduchi katika picha hii umejionea jinsi taaluma inavyofanyakazi katika kazi hii ya usonara wa kimataifa
Ujumbe wa watu wanne kutoka Wadi za Makunduchi ukiongozwa na afisa tawala ndugu Abdallah A. Kombo wa Wilaya ya Kusini umetembelea Manispaliti ya Kiruna, iliyoko kaskazini ya Sweden.
Lengo la ziara hiyo ni kuendeleza ushirikiano ulioanziswa hivi karibuni kati ya Manispaliti ya Kiruna na wadi za Makunduchi. Pande hizo mbili zimekubaliana kushirikiana katika maeneo ya utalii unaojali mazingira (eco-tourism) na elimu.
Watu wengine waliokuwemo katika ujumbe huo ni madiwani wawili, ndugu Hassan kutoka wadi ya Kajengwa, ndugu Zawadi kutoka wadi ya Mzuri Kaja pamoja na msaidizi wa makamo wa pili wa rais, ndugu Mohamed Muombwa.
Ujumbe huo ulitembelea sehemu nyingi za utalii zikiwemo hoteli maarufu iliyojengwa kwa barafu ICE-HOTEL, makumbusho, skuli mbali mbali za chekechea pamoja na sekondari.
Aidha ujumbe wa Makunduchi ulikutana na wafanyabiashara pamoja na jumuiya sizizokuwa za kiserikali, pamoja na kutangaza utamaduni wa Zanzibar katika eneo la uvaaji wa kanga na kofia ya kiua.
Ujumbe wa Makunduchi pia umefanikiwa kuwashawishi wafanyabiashara wa Kiruna kuja kutembelea Makunduchi kutafuta uwezekano wa kuwekeza katika hoteli pamoja na kufungua chuo cha madini kwa ajili ya kusomesha wanafunzi kutoka Afrika Mashariki na kati.
Manispaliti ya Kiruna imejenga Chuo cha Madini cha mfano duniani ambacho huchukuwa wanafunzi kutoka sehemu mbali mbali duniani zikiwemo nchi za Afrika. Kuwepo kwa chuo cha Madini Zanzibar kutasaidia mno wananchi wa Afrika Mashariki kupata elimu ya madini ya kiwango cha kimataifa.
Hatua ya ujumbe wa Makunduchi kutoka nje ya nchi kutafuta uwekezaji imekuja kufuatia wito wa rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein kuzitaka serikali za mitaa nchini kuchangamka kutafuta uwekezaji sehemu mbali mbali duniani. Katika hotuba mbali mbali za Mheshimiwa rais, amekuwa akitoa wito kwa watendaji kuacha kufanyakazi kwa mazoea (business as usual) na badala yake kuwa wabunifu.
Kabla ya ujumbe wa Makunduchi kwenda Kiruna, Sweden, ujumbe wa Kiruna ulifanyaziara Makunduchi mwezi wa Augosti. Ujumbe huo wa watu wanne wa Kiruna uliotembelea skuli za Makunduchi pamoja na sehemu za utalii, kusini na kaskazini ya Zanzibar

No comments:
Post a Comment