Habari za Punde

JKU wafalme mpira wa mikono

Na Mwantanga Ame
 
MAAFANDE wa timu ya mpira wa mikono ya JKU, wamenyakua ubingwa wa mashindano ya ‘Jazera Cup’, baada ya kuwalaza mabaharia waKMKM kwa magoli 23-19. Katika fainali ya michuano hiyo iliyokuwa ikifanyika kwenye uwanja wa Komba wapya Mwembeladu.
 
Mchezo ulikuwa ni wa vuta nikuvute, na hivyo kuwapa burudani nzuri watazamaji.
 
Wadhamini wa mashindano hayo ambao ni Mwakilishi na Mbunge wa jimbo la Rahaleo, walitoa zawadi za jezi seti mbili na fedha shilingi laki mbili kwa JKU na Nyuki iliyoshika nafasi ya pili ili kununulia mipira kumi.


Aidha mgeni rasmi Mke wa Makamu wa Pili wa Rais Mama Asha, alitoa seti ya jezi kwa timu ya wanawake kwa lengo la kuuendeleza mchezo huo.
 
Akitoa nasaha zake baada ya mchezo huo, mgeni rasmi Mama Asha Suleiman Iddi aliaasa vijana kushiriki kikamilifu katika vizuri katikamichezo ili kujenga umoja.
 
Aidha alikemea tabia za baadhi ya vijana zilizoanza kushamkiri sasa kwa kujiingiza katika vitendo viovu vya uvunjifu wa amani, na kusema hali hiyo inaweza kuepukwa kwa vijana wataweza kukaa pamoja na akufanya shughuli za kuinua michezo.
 
Mapema, Mwakilishi wa jimbo la Rahaleo Nassor Salum Ali (Jazeera), alisema ingawa mchezo huo katika Wilaya ya Mjini umeanza kuja juu, bado unakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo za wachezaji kukosa vifaa.
 
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Mikono Zanzibar (ZAHA) Hadi Ubwa Mamboya, aliishauri serikali kuangalia uwezekano wa kujenga uwanja maalumu wa mchezo huo hapo Komba wapya ili uwe na hadhi inayostahili. Mashindano hayo yalishirikisha timu tisa za wanawake na wanaume ambazo ni JKU, KMKM, Nyuki, Fuoni, Mwanakwerekwe,na Kizimkazi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.