Habari za Punde

Kuapishwa kwa Mwakilishi Mpya wa Bububu Bhaa leo

 Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe.Pandu Ameir Kificho akiwasili katika jengo la Baraza tayari kwa kuaza kwa Kikao na Kumwapisha Mwakilishi Mpya wa Jimbo la Bububu Zanzibar akifuatana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
 Mhe Bhaa akifanya taratibu za kuingia katika Ukumbi wa Baraza kwa kula Kiapo cha Baraza akiongozana na Mbunge wa Bububu Sururu wakiwa nje ya ukumbi.
 Mhe. Hussein Ibrahim Makungu akiwa katika nafasi maalum aliyotengewa kabla ya kula kiapo leo asubuhi katika kikao cha baraza kilichoaza leo asubuhi.
 Mhe, Spika wa Baraza la Wawakilishi Pamdu Ameir Kificho akiingia katika ukumbi wa Mkutano wa baraza leo asubuhi.
.
 Mhe Spika akisoma kanuni za baraza kabla ya kuaza kikao na kumuapisha Mhe. Hussein Ibrahim Makungu, kuwa mwakilishi wa Bububu baada ya kushinda katika uchaguzi mdigo wa jimbo hilo mwezi uliopita.
 Mhe. Hussein Ibrahim Makungu( BHAA), akiingia katika ukumbi wa baraza akipishana na Wawakilishi wa Chama cha CUF wakitoka katika Ukumbi wakati akitaka kuapishwa leo asubuhi, kitendo hicho hakikuzuiya kuapishwa kwa Mhe Hussein Ibrahim Makungu(BHAA) 
  Mhe. Hussein Ibrahim Makungu(BHAA) akila kiapo mbele ya Mhe Spika Pandu Ameir Kificho, kabla ya kukaza kwa kikao cha baraza.
  Mhe. Hussein Ibrahim Makungu (BHAA) akitia saini baada ya kumaliza kuapa leo asubuhi.katika ukumbi wa baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar.
Mhe. Hussein Ibrahim Makungu (BHAA)akitowa salamu kwa wajumbe wa baraza baada ya kula kiapo cha kutumikia baraza la wawakilishi, akienda kukaa katika nafasi yake kuaza kwa kikao cha asubuhi leo. 
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakishangilia wakati Wajumbe wa Baraza wa Chama cha CUF wakitoka katika ukumbi wa baraza wakati Mhe. Hussein Ibrahim Makungu(BHAA) akitaka kuaza kuapisha na Mhe. Spika Pandu Ameir Kificho.
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Chama cha Mapinduzi, wakishangilia wakati Wajumbe wa Baraza wa Chama cha CUF wakitoka katika ukumbi wa baraza wakati Mhe. Hussein Ibrahim Makungu(BHAA) akitaka kuaza kuapisha na Mhe. Spika Pandu Ameir Kificho.
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Chama cha Mapinduzi CCM, wakishangilia wakati Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Chama cha CUF wakitoka nje ya ukumbi wa baraza wakati Mhe. Hussein Ibrahim Makungu(BHAA) akiapishwa leo asubuhi. na Mhe. Spika Pandu Ameir Kificho.
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Chama cha CUF, wakirejea katika ukumbi wa Mkutano wa Baraza baada ya kumaliza kuapishwa Mwakilishi mpya wa jimbo la Bububu Mhe. Hussein Ibarahim Makungu (BHAA) wakipinga ushindi wake alioupata katika uchaguzi mdogo wa jimbo la bububu uliofanyika mwezi uliopita.
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Chama cha CUF, wakirejea katika ukumbi wa Mkutano wa Baraza baada ya kumaliza kuapishwa Mwakilishi mpya wa jimbo la Bububu Mhe. Hussein Ibarahim Makungu (BHAA) wakipinga ushindi wake alioupata katika uchaguzi mdogo wa jimbo la bububu uliofanyika mwezi uliopita.
Mhe. Makame Mshimba wa Jimbo la Kitope akishangilia kuingia kwa wajumbe wa CUF katika ukumbi wa mkutano.
Waheshimiwa wakishangilia ikiwa ni ishara ya ushindi  wa Mwakilishi wa Jimbo la Bububu kwa ushindi wake wakati wa kuapishwa leo asubuhi. 
Mhe Hussein Ibrahim Makungu akiwa katika sehemu yake baada ya kuapishwa leo asubuhi.
Ukumbi ukiwa na mapengo ya hapa na pale baada ya Wajumba wa Baraza la Wawakilishi wa Chama cha CUF kususia kuapishwa kwa Mhe Hussein Ibrahim Makungu(BHAA) kwa ushindi wake alioupata katika uchaguzi mdogo wa jimbo la bububu uliofanyika mwezi uliopita.















2 comments:

  1. Huyo mwakilishi kakalia 100% feki no debatable na hao wafuasi wa ccm wanaofurah kwa taarifa yenu mnajipalilia makaa wenyewe kama pweza mupooo!!!!!!!!kanza hata kuvaa hajui kavaa suti ovyoo na huko miguuni yote imejaa mavumbi na imechanika chanika halafu ndo anaapishwa hapo si bora angevaa kanzu na koti simple.

    ReplyDelete
  2. HAHAHAHHAH Du!!! huyu Bhaa kawa Mwakilishi!! sasa Disco watatupugia nani?? Ama kweli Zanzibar ukijikaza kidogo tuu unakuwa Muheshimiwa, kesho kutwa mtasikia huyu Habiba Mapaip kawa Mbunge.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.