Habari za Punde

Picha na Matukio kutoka Pemba

 
Kundi la waandishi wa habari wa vyombo mbali mbali Kisiwani Pemba wakiangalia kikuta kilichosadikiwa kuwekwa na wakoloni tokea miaka ya 1954 katika eneo la Tunduawa ambapo panasadikiwa kuwa pana nishati ya mafuta. Mwenye mkoba ni mwandishi Mariyam Nassor akiangalia kwa kina baada ya kuwepo kwa uchaba wa mafuta kwenye kikuta hicho (picha na Haji Nassor, Pemba)

 
Mbunge wa Jimbo la Ole Rajab Ali Mbarouk (katikati) akishirikiana na Kikundi cha usafi wa mazingira kilichopo Wawi (Task Force Environment), na sober House ya Chake chake wakati kikundi hicho kilipofanya usafi katika Hospital kuu ya Chake chake ikiwa ni kawaida ya kikundi hicho kufanya usafi wa mazingira kila siku (picha na Haji Nassor, Pemba)


Mwandishi wa Shirika la Magazeti linalochapisha Gazeti la Zanzibar Leo na Zanzibar Leo Jumapili Haji Nassor, wakati akimkabidhi magazeti Mwenyekiti wa Jumuia ya Maendeleo ya Wanawake ya Tundauwa Shehia ya Kilindi Wilaya ya Chake chake, wakati timu ya waandishi walipofika kijiji huko ili kuandika habari za vijijini (picha na Is-haka Mohamed)  

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.