Migogoro ya ndoa bado kikwazo, watoto ndio
waathirika wakubwa
Na Haji Nassor, Pemba
TABIA ya wanawake kutelekezwa na kisha kunyang’nywa
mali hasa baada ya kuachwa, imekuwa ni tatizo sugu hapa visiwani, licha ya
taasisi mbali mbali kupigia kelele suala hilo .
Tabia hii ambayo
mwishowe huwaweka mazingira magumu wanawake na watoto wetu, imekuwa ikifanyika
bila ya aibu kwenye jamii zetu ambazo zinawasomi waliobobea wa kila nyanja na
kila fani.
Kitabu kitakatifu
cha Quran kimeleeza wazi kwamba ‘daima hawawi sawa kati ya aliesoma na asie
soma’’ hili kwa haraka haraka ni rahisi kulitafisiri lakini vitendo vyake
huchekeshwa kwa jamii yetu.
Wapo wanaume huoa
kwa furaha, shangwe, ngoma, nderemo na vifijo vikiambatana na nyimbo na udi wa
asumini, mwanamme akiamini kwamba kampata amtakae kwenye ndoa.
Sawa, lakini mbona
kadri siku zikisongo mbele kuna vitendo vya ukatili na utelekezaji kwa mpendwa
wako, tusemeje uliomuoa kwa mkataba kwamba akianza kupoteza uzuri wake umtenge
na kumkosesha baadhi ya huduma, kama ni hivyo
,sio sahihi.
Leo tumekuwa
tukishuhudia korja za kesi katika vyombo vya sheria ambazo zinahusiana na
wanawake na watoto kutelekezwa na hasa baada ya mwanamme kutoa talaka.
Ukubwa wa tatizo
untaisha hasa kwa vile wakosaji hawatiwi adabu kama
wao wanavyowatekeleza wanawake na watoto na kuwaacha bila ya msaada wowote.
Kwa mfano Wilaya
ya Chake chake Kisiwani Pemba, kwa mwaka 2011 kuliripotiwa kesi 18 ambazo zote
zinahusiana na utelekezwaji wa wanawake na watoto, na kesi mbili (2)
zilihusiana na kudai mahari.
Kesi sita (6)
zilihusiana na kudai mali
baada ya mwanaume kuchuma mali
kisha kumtolea nje mwanamke ambae kama
nilivoeleza awali alimumoa kwa udi na asumini.
Pia Wilaya ya
Chake chake katika mwaka huo wa 2011 kulikua na kesi mbili (2) zinazohusiana na
migogoro ya familia ingawa sulhu kwa kesi hizi ilipatikana na wanamue kuanza
kupeleka huduma.
Matendo haya ni
yale tu wanawake walioshindwa kuvumilia na kuamua kuyafikisha Wizarani, mbali
ambayo hayakuripotiwa kwa sababu mbali mbali ikiwa ni pamoja na kuona aibu na
haya.
Lakini suala la
utelelezaji wa familia kwa wanaume pia kulikua na kesi nane (8), na sulhu nayo
ikapatikana , ambapo kwa Wilaya Mkoani kulikua na migogoro miwili (2) ya ndao
na ufumbuzi ilipatikana .
Kutokana na
wanaume kuwatelekeza wake zao na watoto, Wizara ya Uastawi wa Jamii Maendeleo
ya Vijana, Wanawake na Watoto imekua ikipokea shilingi 139,000/= toka kwa
wanaume sita ambao walilalamikiwa Wizarani hapo.
‘Shilingi laki
moja zaidi, kila mwezi tunakusanya na kuwakabidhi wanawake ambao walikuwa
tayari wameshatelekezwa na waume zao kwa kutopatiwa huduma mbali mbali
humibu’’,alisema Afisa Maendeleo ya Wanawake na Watoto Wilaya ya Chake chake
Salma Khamis Haji alipokua akizungumza na mwandishi wa makala haya.
Afisa huyo alisema
miongoni mwa sababu inayopelekea wanaume kuwatelekeza wanawake na watoto ni
kusahau wajibu wao baada ya kufunga ndoa.
‘’Wanaume,
wanaamua kuoa wakiwa hawajai thamani ya ndoa wala thamani ya mwanamke na watoto,
hivyo ni mwepesi kuwatelekeza na kuwakatia huduma za lazima ‘’,alisema Salma.
Kwa mujibu wa takwimu
zilizotolewa na Wizara ya Ustawi wa Jamii Maendeleo ya vijana, Wanawake na
Watoto Pemba, ilionyesha kulikuwa na makosa 51 ambayo yaliripotiwa kwa upande
wa Mkoa wa Kusini Pemba .
Kati ya makosa
hayo yamo ya udhalilishaji na utelekezaji wa wanawake na watoto, Wilaya ya
Chake chake pekee ilibeba makosa 38 na 13 Wilaya ya Mkoani.
Kwa mfano kulikua
na kesi ya kuwafungia ndani watoto wawili ,ambayo ilifikishwa kituo cha Polisi
cha Chake chake Juni, 2011, (no CHC /PCR.136) ambayo baada ya wazazi kuaicha
Serikali ililamikia, lakini kutokana na kukosa ushirikiano na wahusika, Julai,
17, ilifungwa na RCO Kusini Pemba .
Katibu wa Mtandao
wa Polisi wanawake Kusini Pemba Sajenti Zuwena Hamad Ali, alisema baadhi ya
wazazi wamekuwa wakishindwa kushirikiana
vyema na vyombo vya kisheria zinapotokezea kesi za aina hii.
‘’Sisi Dawati la
wanawake na watoto na hata Jeshi la Polisi tumekuwa tujitahidi kuzifuatilia
kesi za aina hii, lakini kesi ikianza kuwa nzuri mashahidi huingia mitini na
kutuvunja moyo’’,alisema Sajent Zuwena.
Kadhi wa mahakama
Wilaya ya Chake chake Daud Khamis Salum yeye alisema suala la wanawake
kunyang’anywa mali
baada ya kuacha lipo kwa kiwango kikubwa kutokana na wanake kutofahamu haki zao.
‘’Kitabu
kitakatifu cha Qur-an ,kimeeleza wazi kwamba vi vyema wanawake wakapewa haki
zao mara anapoaachwa ili iwe nusra katika maisha yake’’,alisema Kadhi huyo.
‘’Kitoka nyumba ‘sheikh’
ni lazima na ni wajibu kwa mwanamme kumpa alie kuwa mke wake, hata kama hakuchangia, ilimradi iwe umekichuma wakati ukiwa na
mke tu……….wapewa chao’’,alisema huku akinukuu aya ya Qu-ran.
Kuna kesi 18
zizazohusiana na migogoro ya ndoa na wanawake na watoto kutelekezwa, ambapo
ndoa hizo pia zimeshavunjwa na Mahakama ya Kadhi kwa mujibu wa sheria na mamla
ilionayo.
Kadhi hakusita kueleza
kuwa, wanawake na watoto waliotelekezwa moja kwa moja ni kesi 12, ambazo zimejumuisha
watoto 30 na hatua za kisheria zilichukuliwa kwa mujibu wa taratibu.
Kwa upande wa
shehia ya Msingini Wilaya ya Chake chake kulikuwa na kesi tatu (3) ambazo
wanawake na watoto walitekezwa na waume ,kwa sababu mbali mbali ikiwa ni pamoja
na uhamisho wa kikazi.
Mzee Juma Seif ni
sheha wa shehia hiyo, alisema sababu kubwa inayofanya baadhi ya wanaume kuzitelekeza
familia zao ni pamoja na kuoa zaidi ya wake wawili na kukosa kuelewa wajibu
wao.
‘’Wapo wanaume
ambao wakiongeza mke tu, hujaribu kuzitelekeza familia zao bila ya kujali
athari zake’’,alifafanua sheha huyo.
Hata hivyo alisema
kesi za aina hiyo haziripotiwi ipasavyo kutokana na wanawake kuogopa kuachwa na
wanaume zao na kusemwa na jamii husika.
Mkuu wa Wilaya ya
Chake chake Mwanajuma Majid Abdallah alisema kesi za kuwatelekeza wanawake na
Watoto na kuwakosesha mali
naada ya kuachwa, hufanya na wanaume kutokana na kutowapendelea maendeleo.
Fatuma Sahibu Ali
wa kijiji cha Kilimahodi Wilya Chake
chake ambae alitelekezwa na mumewe, na
kwa sasa amekuwa akichukua fedha Wizarani kutokana na kutopewa huduma za lazima
na aliekuwa mumewe .
Kesi za wanawake
na watoto kutelekezwa na kunyang’anywa mali haziripotiwi ipasavyo katika vyombo
mbali mbali huku sababu ikitajwa kuwepo kwa mzunguruko wa taratibu za kufuatlia
kesi hizo
No comments:
Post a Comment