Na
Masanja Mabula, Pemba
MOTO
wa ajabu unaotokea katika mazingira ya kutatanisha bado unaendelea kuteketeza
nyumba na mali za wananchi wa kijiji cha Tumbe Mashariki, jimbo la Tumbe,
wilaya ya Micheweni, Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Moto
huo ambao ulianza kuteketeza tokea Septemba 28 mwaka huu , tayari umeteketeza
nyumba zipatazo 13 hadi sasa huku baadhi ya nyumba nyingine zikishuhudiwa vitu
vya ndani kama nguo zikiungua huku
makabati yakibakia salama.
na magodoro z ndivyo vinavyoteketea na nyumba
kubaki salama .
Wakizungumza
na mwandishi wa habari hizi baadhi ya wakaazi wa kijiji hicho walisema moto huo
umekuwa ukitokea kutokana na imani za kishirikina.
Walisema
wananchi wa kijiji hicho wamepatwa na hofu kubwa, kwa sababu moto huo hutokea
katika mazingira yasiyotarajiwa.
Moto
huo umesababisha hali ya umaskini kutokana na wananchi kutumia muda wao mwingi
ewakiwa nyumbani wakisubiri kukabiliana na moto huo pindi unapotokea.
Wananchi
hao walisema tokea kuanza kutokea moto
huo siku ya Ijumaa ya wiki iliyopita shughuli za kiuchumi zimezorota kwani
wamekosa hata muda wa kushughulikia masuala ya uzalishaji mali jambo
ambalo limekuwa ni kikwazo katika kujiletea maendeleo.
"Matukio
haya kwa kweli yansababisha hali ya umaskini katika familia zetu kwani
tunashindwa hata kwenda baharini kuvua, na hata watoto wetu wanakosa muda wa
kujisomea kutokana na wasiwasi uliotanda juu ya usalama wa maisha kwa vile
hatujui moto utatokea wakati gani,” alisema Khamis Salim Kombo.
Aidha
alisema cha kushangaza zaidi ni kuona wakati mwengine kunaungua nguo na vitu
vingine lakini mapaa ya nyumba yanabakia salama licha ya moto huo kukiripuka hadi
kwenye mapaa.
Alisema
katika tukio lililotokea katika nyumba yake bahasha ya nguo zilizokuwa
zimeandaliwa kwa ajili ya kwenda kuoshwa ziliwaka na kuteketea pamoja na godoro huku kitanda kikibaki salama
jambo ambalo limewaweka katika wakati mgumu wa kujua chanzo cha moto huo .
Udadisi
uliofanywa na mwandishi wa habari hizi kwa kuzungumza na wazee alipofika
katika katika kijiji hicho wakati wa moto ukiendelea kuwaka , walisema
kuwa zipo taarifa tofauti juu ya chanzo cha moto huo ambazo zinahusishwa na
masuala ya imani za kishirikina
kulikosababishwa na kusahauliwa kwa masuala ya kijadi.
Ikiwa
katika eneo la tukio gazeti hili lilishuhudia nyumba ya mzee Khatib Omar Kombo
alikiwaka moto wakati mwenyewe akiwa amekwenda msikitini na wala hakukuwa na
dalili zozote za kuwepo moto ndani ya nyumba hata hivyo wananchi waliwahi na
kuuzima moto huo kabla ya kuleta madhara.
Taarifa
zisokuwa rasmi zinasema kuwa chanzo cha
moto huo ni kukatwa mwembe kwa ajili ya kupisha ujenzi wa soko kijijini hapo
huku chanzo chengine cha habari kikieleza kuwa baadhi ya wazee walipewa fedha
kwa ajili ya kununua ng’ombe wa mji lakini
hawakutekeleza ahadi hizo.
Akizungumza
na wananchi wa kijiji hicho Kamanda wa Polisi mkoa wa Kaskazini Pemba, Kamishna
Msaidizi Mwandamizi, Yahya Rashid Bugi aliwataka wazee hao kuondoa imani za
kishirikiana na kwamba njia pekee ya kuweza kuondoa tatizo hilo ni kwa wananchi
hao kuongeza idaba,maombi na dua.
"Acheni
kuamini masuala ya kishirikiana kuhusiana na matukio haya, nawaombeni kuwa njia
pekee ni kuongeza ibada, maombi, dua na sala
na kwamba hii ni mitihani kutoka kwa Allah , endeleeni kuwa wavumilivu,"
alishauri Kamanda Bugi.
Kufuatia
kuwepo na matukio hayo wananchi wa Tumbe Mashariki katika kijiji cha Kaliwa
wameandaa maombi maalum kwa ajili kuomba kuondoshewa kwa kadhia hiyo ambayo
imenaweka roho za watu juu na kwapa wasi wasi juu ya mustakabi wa maisha yao na
mali zao.
Kijiji cha Tumbe kilikuwa maarufu sana kwa
masuala ya matambiko ya kijadi kila mwaka, kama
ilivyo kijiji cha Makunduchi.
No comments:
Post a Comment