Habari za Punde

Waandishi watishiwa maisha na vijana wanaofanya vurugu

 Na Salma Said
 
Waandishi wa habari waliopo mjini Zanzibar wanaofuatilia ghasia zinazoendelea hapa wamekuwa kwenye hatari kwa kutishiwa maisha yao na vijana wanaofanya vurugu.
 
Makundi yanayofanya vurugu yako ya aina tatu Ubaya ubaya, Kimya kimya na Mbwa mwitu hufanya vurugu na kupora watu mali zao wakiwemo kwenye vyombo vya usafiri na kuvamia mabaa.


Waandishi hao wakiwemo wa kimataifa walivamiwa na kundi la vijana na kuwekwa chini ya ulinzi eneo la Mbuyuni na kutaka kunyang'anywa vifaa vyao vya kazi lakini waliokolewa na walinzi waliokuwa jirani.
 
Waandishi walivamiwa katika eneo la Mbuyuni baada ya kumaliza kusali sala ya Ijumaa ambapo waandishi hao walitakiwa kuondoka na kutishiwa maisha yao kwa kupigwa ambapo baadhi yao walisukumwa na kupigwa.
 
“Mimi nimeshachoka kupigwa na hawa watu lakini niliyempiga ninamjua na kwa kweli kwa sasa hatukubali tena” alisema Munir Zakaria mwandishi wa Channel Ten.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.