Habari za Punde

Vipindi vya Uamsho vyapigwa marufuku

 
Katika hatua nyingine Tume ya Utangazaji ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imepiga marufuku vipindi vyote kwenye redio na televisheni vya kikundi cha dini cha Uamsho.
 
Barua iliyotumwa jana kwa Wakurugenzi wa vituo vya redio na televisheni vya hapa ilisema kwamba hatua hiyo imetokana na ghasiza zinazoendelea nchini ambazo inasadikiwa kuwa zinachochewa na kikundi hicho.
 
Barua hiyo iliyosainiwa na Mtumwa B Mzee kwa niaba ya Katibu Mtendaji wa Tume ya Utangazaji ilisema kwamba itawachukulia hatua wale wote watakaokaidi agizo hilo
 
 
.
 

1 comment:

  1. Assalam Alayikum ndugu Mapara,
    eti Serikali kuwataka wakurugenzi Wa Vyombo vya Habari/TV Kutokutangaza vipindi vyote vya Uamsho hata habari zao Jee !! Vyombo vya Habari vitakuwa na uhuru wa kutangaza mambo wanayo yataka ya kuelimisha au kuhabarisha matukio yanayoendelea hasa kwa sisi watu wa mashamba ama ndio Haturuhusiki Kusikia kinacho endelea huko Mjini

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.