Asalaam alaikoum Wazanzibari wote popte walipo
duniani.
Kwa niaba ya Interim President na Katibu wa
Zanzibar-Canadia Diaspora Association, chini ya usajili rasmi katika serikali
ya Ontario kama Zacadia Foundation, nachukuwa fursa hii kuiwasilisha na kuitambulisha
LOGO yetu mpya ya Jumuia yetu hapa Toronto na Canada kwa jumla.
Baada ya proposal mbali mbali zilizofanywa na
kufanyiwa uhakiki, kwa msaada wa ndugu yetu ambaye ni msanii wa mambo ya
Graphic, hatimaye nimeweza kufanya Logo hii ambayo itatumika rasmi kama
alama ya
Zanzibar-Canadian Diaspora Association (ZACADIA) na Zacadia Foundation.
Baada ya mafanikio hayo, htauna budi kutoa shukrani
zetu za dhati kwa msanii wetu huyu,
ndgu Mohammed Khamis kwa kazi yake nzuri, kwa kushirikiana na mmoja wa
volunteer wa ZACADIA hata kufikia kupatikana kwa logo hii ambayo tunahisi ni
nzuri zaidi ya zile za nyuma.
Wakati huo huo, tunapenda kuwaarifu Wazanzibari wote
duniani kwamba, ZACADIA Foundation imebuni mradi wa kijamii kwa ajili ya
kuwasaidia watoto mayatima na masikini wa vijijini Unguja na Pemba kwa
kuwapatia nyenzo muhimu za maisha kama vile nguo, chakula, vifaa vya skuli
usafiri kwa wale walio mbali na skuli kama baiskeli pamoja na huduma za
kuangaliwa kiafya.
Mradi huu umekusudiwa kuwashirikisha Wazanzibari walio nje
na ndani ya Zanzibar kwa kuchangia kwa njia moja au nyengine katika kufanikisha
kuwasaidia watoto hao ambao tayari tunao kumi kwa sasa, watano kutoka kila
kisiwa, Unguja na Pemba.
Mbali na michango mbali mbali ya kawaida, ZACADIA
imekusudia kuwatafuta wadhamini wa watoto hao kila mmoja mtoto mmoja au zaidi
ya mtu mmoja kumdhamini mtoto mmoja kwa kutoa mchango wa dola 30 kwa mwezi ili
kudhamini motto kufaniksha kupatiwa huduma hizo tulizozitaja hapo juu.
Pamoja na Sponsorship hiyo, ZACADIA itafanya juhudi
ya kutafuta fedha zaidi ili kuongezea kuwahudumia watoto hao kumi wa kuanzia
mpaka motto huyo atakapomaliza sekondari.
Ikiwa wakiristo wanatoa misaada kama hii kwa watoto
wa wenzao katika nchi zinazoendelea, kwa nini sisi Wazanzibari tushindwe
kuwasaidia watoto wetu wenyewe kwa kupitia njia kama hizo ambazo ZACADIA
inataka kuzianzisha kwa jamii za Wazanzibari.
Kwa wle ambao watakuwa tayari kuanza kutoa michango
yao kwa ajili ya mradi huu, watuandikie infozacadia@gmail.com ili tuanze kutayarisha mipango kabambe
ya namna ya kutuma michango yao kwa njia ya salama kupitia PayPal. Mpango
mzaima umi mbioni kutayarishwa ili kukamilisha website ambayo itarahisisha
Mradi huu kuanza na wachangiaji kuweza kusaidia.
Nimeshuhudia Wazanzibari wakitoa dola 30 kila mwezi
kupitia World Vision ili ku sponsor mtoto. Sasa tushirikiane sisi wenyewe
tuweze kuufanikisha mradi huu kwa ajili ya watoto wetu ambao hawajawahi
kupatiwa misaada ya aina hii ambayo huishia Tanganyika.
Ni matumaini yetu kwamba Wazanzibari, pamoja na
marafiki zao, watautangaza mradi huu na watajitokeza kwa wingi kuchangia na ku
sponsor watoto hawa kumi tulionao kwa sasa.
ZACADIA inakusudia kumuunganisha mtoto Nairat katika
mradi huu mara mipango itakapokamilika.
ZACADIA inatoa shukrani kwa wale Wazanzibari waishio
Toronto na viunga vyake (GTA) kwa michango yao ambayo waliitikia wito wa wa
ZACADIA katika kumchangia NAIRAT na dada yake Bisambe ili waokolowe kwa uwezo
wa Mwenyezi Mungu kutokana na maradhi yaliyowakumba.
Mwisho, hatuna budi kutoa shukrani kwa ndugu Othman
Maulid na Blog yake ya ZANZINEWS, Bi. Salma Said na uongozi wa MZALENDO.NET kwa
juhudi zao walizozifanya katika kuwaelimisha na kuwapa taarifa mbali mbali za
Wazanzibari duniani kote.
Nwasilisha kwa niaba ya:
President na Katibu
ZACADIA
No comments:
Post a Comment