Habari za Punde

Idara ya Makumbusho na mambo ya kale yahamasisha utalii kwa wote

 Wasanii wakiingia kwenye Pango la kihistoria linalo sadikiwa kuguliwa na Kijana aliekuwa akichunga Mbuzi baada ya Mbuzi wake Mmoja kuingia ndani ya Pango hilo.
 Maalim.Ramadhan Ali Machano kaimu mkuu makumbusho na Mkuu wa huduma za elimu Idara makumbusho na mambo ya kale alie juu ya jukwaa akiwapa historia ya Beit el Ajaib Wasanii mbali mbali wa Zanzibar wakiongozwa na Maalim Haji Mkadam kutoka Baraza la Sanaa Zanzibar wakiwa katika ziara ya kutembelea sehemu mbali mbali za kihistoria,kuhamasisha Utalii wa ndani kwa wananchi.
 Maalim.Ramadhan Ali Machano kaimu mkuu makumbusho na Mkuu wa huduma za Elimu Idara makumbusho na mambo ya kale akiwafahamisha kitu wasanii hao juu ya Kasir la Mtoni lililojengwa na Sultan Seyyid Said mnamo mwaka 1828.
 -Wasanii wakitizama Mahandaki ya vita vya Pili vya Dunia mwaka 1939-1945 huko Mangapwani yaliojengwa na Waengereza yalitumika kama sehemu ya kujihami.
Mkuu wa ziara hiyo kutoka Idara ya Makumbusho na mambo ya Kale Bi.Zuhura Ali Juma akitoa shukran zake kwa wasaii hawapo pichani walio tembelea sehemu mbali mbali za kihistoria akiwaomba wawe washajihishaji wakubwa wa Utalii kwa wate.
PICHA NA MAKAME MSHENGA-MAELEZO ZANZIBAR.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.